Dalili gesi asilia zaonekana kitalu cha Lindi – Mtwara

MTWARA: UTAFITI unaoendelea kufanyika katika Kitalu cha Lindi–Mtwara, mkoani Mtwara umeonesha dalili za uwepo wa gesi asilia, hususani katika vijiji vya Mnyundo na Mpapura, ambapo visima vya maji vilibainika kuvujisha gesi asilia.

Utafiti huo unajumuisha jumla ya vijiji 48 katika eneo la takriban kilomita za mraba 736 ambapo vijiji 40 vinatoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara (Mtwara DC) na vijiji vinane ni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtama (Mtama DC).

Katika ziara yake ya kukagua miradi ya gesi na mafuta mkoani Mtwara, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk James Mataragio, amesema kuwa utafiti wa awali unaonesha uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa gesi asilia katika eneo hilo.

“Kwa kutumia data za mitetemo zilizokusanywa awali, tumebaini kwamba kuna hadi asilimia 32 ya uwezekano wa gesi kuwepo katika kitalu hiki,” amesema Dk Mataragio.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button