Oginga ateuliwa Kaimu Kiongozi wa ODM

KENYA : SENETA wa Siaya, Oburu Oginga, ameteuliwa kuwa kaimu kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kufuatia kifo cha mdogo wake, Waziri Mkuu wa zamani Raila Amolo Odinga.

Uamuzi huo umefikiwa Alhamisi asubuhi katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, ambapo wajumbe walikubaliana kwa kauli moja kwamba Oginga aongoze chama kwa muda hadi mikutano ijayo itakapopanga mustakabali wa uongozi wa kudumu. SOMA: Odinga kugombea uenyekiti wa Tume AU

Rais William Ruto ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa, huku bendera ya taifa ikipeperushwa nusu mlingoti kwa heshima ya Odinga, ambaye atazikwa Jumapili hii nyumbani kwake Bondo, Kaunti ya Siaya.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button