Odinga kugombea uenyekiti wa Tume AU

KENYA : WAZIRI Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga, amepanga kushiriki katika mdahalo wa kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) utakaofanyika katika Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 13 Desemba 2024.

Katika mdahalo huo, Raila atachuana na wagombea wawili wengine akiwemo Mahmoud Ali Youssouf kutoka Djibouti na Richard Randriamandrato kutoka Madagascar.

Mdahalo huu ni sehemu ya mchakato wa awali kabla ya uchaguzi rasmi wa Februari 2025, ambapo atachaguliwa mrithi wa Mwenyekiti wa sasa wa Kamisheni ya AU,Moussa Faki Mahamat kutoka Chad.

Advertisement

Kwa upande wa Raila amesema kushiriki kwake katika mdahalo huu ni hatua muhimu katika kuimarisha nafasi yake katika kinyang’anyiro hiki cha kimataifa. SOMA: ‘Umoja wa Afrika usaidie kumaliza ugaidi EAC’