SUA yapata miradi 36 ya bil 10.5/-

MOROGORO: CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA ) kimeeleza kuwa hadi kufikia Oktoba mwaka huu, miradi mipya ya utafiti 36 yenye thamani ya Sh bilioni 10.5 imepatikana.
Kati ya miradi hiyo 10 inafadhiliwa na wafadhili wa nje, miradi miwili ya Serikali kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na miradi 24 inafadhiliwa na Chuo Kikuu hicho kupitia mapato yake ya ndani.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu hicho, Andrew Massawe amesema hayo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Chuo hicho, Jaji Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba wakati wa mahafali ya 46 ya Chuo Kikuu hicho yaliyofanyika Kampasi ya Edward Moringe mkoani Morogoro.
Massawe amesema tafiti hizo zimeendelea kuchangia katika kukuza maarifa na kutatua changamoto katika sekta za kilimo, mifugo, mazingira na maendeleo ya jamii.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu hicho amesema baraza linaendelea kusimamia mikakati ya kuimarisha vyanzo mbadala vya mapato ya ndani kuoitia miradi ya kibiashara , ushauri wa kitaaluma na uwekezaji katika maeneo ya kimkakati.
Amesema katika kutekeleza jukumu la usimamizi wa shughuli za utafiti, baraza linaendelea kuhimiza matumizi ya matokeo ya kitafiti zinazofanywa chuoni kuchangia katika sera na mipango ya maendeleo ya taifa.
Massawe pia amesema baraza hilo linasimamia kwa karibu shughuli za ugani na ushauri unaotolewa na Chuo Kikuu hicho kwa wadau mbalimbali hususani katika sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi , mazingira na maendeleo vijijini.
Amesema hadi sasa wadau 79,147 wamenufaika na huduma hiyo wakiwemo wakulima , wafugaji, watafiti, maofisa ugani na watumishi kutoka sekta binaafsi na sekta za umma ambapo asilimia 48 ya wanufaika walikuwa ni wanawake.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Raphael Chibunda amesema katika mahafali hayo jumla ya wahitimu ni 3,560 wakiwemo wanaume 2,029 na wanawake 1,531.
“ Kwa kawaida kuhitimu katika Chuo Kikuu SUA haijawahi kuwa lele mama , na kwa dhati ya moyo wangu ninayofuraha kuwapongeza wahitimu wote “ amesema Profesa Chibunda.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho alitaja wahitimu wa shahada ya kwanza walikuwa 3,275 kati yao wanaume 1,861 na wanawame 1,413, shahada za umahili 127 kati yao wanaume 76 na wanawake 51.
Profesa Chibunda alitaja wahitimu mwengine 18 walikuwa ni wa shahada uzamivu (PhD) na kati yao wanaume 12 na wanawake sita , wahitimu wa stashahada 100 na wahitimu wa Astashahada 38.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho amesema katika mahafali hayo wanawake ni 1,531 ambao ni sawa na asilimia 42.95 ya wahitimu wote .
Akizungumza baada mahafali hayo, Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu hicho (2025/ 2026), Shahidu Iddy aliwaasa wahitimu hao kutumia elimu yao, ujuzi na maarifa yao kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii kupitia taaluma waliyonayo na waliyoipata kutoka SUA.
Google pays $220 an hour online. My close relative had been unemployed for nine months, but last month, she received a $25k paycheck by working from home for 10 hours a day. Everyone should try this job now—just use this link.
COPY THIS →→→→ http://Www.Work99.Site
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com