Mishahara juu sekta binafsi

SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeongeza kima cha chini cha mishahara kwa sekta binafsi kwa asilimia 33.4, itakayoanza kutolewa rasmi Januari Mosi, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amesema kima cha chini cha mshahara kimeongezeka kutoka Sh 275,060 hadi Sh 358,322.

Ameema amri ya kima cha chini cha mshahara imegusa sekta ya kilimo, afya, mawasiliano, usafirishaji, hoteli, madini, biashara na viwanda.

Nyingine ni shule binafsi, huduma za ulinzi binafsi, nishati, uvuvi na huduma ya baharini, michezo na utamaduni pamoja na huduma nyinginezo, huku wafanyakazi wa majumbani na sekta ya ujenzi zikiwa hazijajumuishwa katika ongezeko hilo.

Mei Mosi, 2025 Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Singida, alitangaza kupandisha mishahara ya watumishi wa umma kwa ongezeko la asilimia 35.1 na kima cha chini kiliongezeka kutoka 370,000 hadi Sh 500,000.

Amesema Sheria ya Taasisi za Kazi, Sura 300 humpa dhamana waziri kuunda Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara kwa ajili ya kufanya utafiti na kushauri kuhusu viwango vya chini vya mshahara na mapitio hayo hufanyika kila baada ya miaka mitatu, huku tangazo la mwisho lilitolewa mwaka 2022 lililoanza kutumika Januari Mosi, 2023 na kumalizika Desemba 2025.

Ridhiwani alisema amri ya kima cha chini cha mshahara imetangazwa kupitia Gazeti la Serikali la Oktoba 13, 2025 yanye Namba 605A.

“Kwa mujibu wa amri hiyo, sekta binafsi kima cha chini cha mshahara zimeongezeka kutoka 13 za 2022 hadi 16 kwa 2025 na kutoka sekta ndogo 25 za 2022 hadi 46 kwa 2025 kima cha chini cha mshahara kimeongezeka kwa wastani wa asilimia 33.4 kutoka Shilingi 275,060 hadi Shilingi 358,322,” alisema.

Kadhalika, Ridhiwani alitoa msisitizo kwa waajiri wa sekta binafsi kuzingatia takwa hilo la kisheria na kutekeleza kima hicho kipya cha mshahara, mara kitakapoanza kutumika rasmi.

“Ofisi yangu itaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa amri hii, kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi pamoja na kufanya tathmini ya mara kwa mara ili kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kikamilifu… ofisi yangu haitasita kuchukua hatua kwa waajiri watakaokaidi au kushindwa kutekeleza amri hii kwa makusudi, alisisitiza.

Ongezeko hilo limetokana na mapitio ya vigezo vilivyoainishwa ndani ya mikataba ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), ikiwemo uwezo wa waajiri kulipa, kupanda kwa gharama za maisha, uwezo wa waajiri katika kuendesha biashara  zao kwa tija pamoja na dira ya maendeleo ya nchi katika kukuza uchumi, ajira na kazi zenye staha.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button