Serikali yapongezwa ukamilishaji miradi mikubwa

MOROGORO: TAASISI ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere imeipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati ukiwemo wa kufua umeme kutoka Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) wa megawati 2115 na kukamilisha malipo yote ya mkandarasi kulingana na mkataba.
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ,Peter Mavunde ametoa pongezi hiyo baada ya kupata taarifa ya mradi huo kutoka kwa Mkurugenzi wa JNHPP wakati wa ziara ya viongozi wa taasisi hiyo kwenye Bwawa la Nyerere ikiwa ni hitimisho la maadhimisho ya kumuenzi Baba wa Taifa kwenye shughuli za Nyerere Day zilizofanyika Oktoba 14, 2025.
“Tunaishukuru Serikali kwa kutupatia fursa ya kutembelea mradi huu mkubwa wa kitaifa na wenye heshima ya pekee katika nchi yetu, Afrika na hata dunia zima,” amesema Mavunde.
Mavunde amesema kuwa ,taasisi inaipongeza Serikali kwa kuwa mradi huo mkubwa kutokana na kwamba umetumia fedha za Watanzania wenyewe na kitendo hicho kinaliwezesha taifa kuendelea kusimama kidete.
Pia amesema kuwa,Taasisi imesifu baada ya kuona watu wote wanaosimamia uendeshaji wa mradi huo mkubwa ni wataalamu wabobevu wakutoka hapa nchini ambao ni vijana.
“Tumetembelea eneo la mitambo na tumeona taaluma inavyofanya kazi ya ajabu kwa ustawi wa nchi yetu kwa maana wataalamu wanaosimamia ni vijana wadogo na hii inaweka imani ya kwamba vijana wetu wana uwezo mkubwa kufanya kazi za kitaifa na za kimataifa,“ amesema Mavunde .
Hivyo kutokana na hayo amesema, taasisi inatoa rai na ushauari kwa Serikali, vijana hao wapewe motisha ,si lazima fedha hata mafunzo zaidi ili waweze kuendelea kufanya kazi zao vizuri zaidi na kuokoa nguvu kazi yenye umuhimu mkubwa katika taifa letu.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Idara ya Maadili na Ushauri ya Taasisi hiyo na Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Zainabu Mbilo amewapongeza marais wote wa awamu zilizopita kwa kuendelea kusimamia maono ya Baba wa Taifa kuhusu eneo hilo.
Mbilo amewataja miongoni mwao ni Hayati Dk John Magufuli ambaye aliuanzisha ujenzi wa mradi huo na baadaaye alipofariki dunia umeendelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita ya Dk Samia Suluhu Hassan hadi kukamilika kwake .
Kwa mujibu wa Wizara ya Nishati pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)kuwa mradi huo umegharimu zaidi ya Sh trilioni 6.5.
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website
Open This…. https://Www.work99.site