HESLB yafafanua waliopata mikopo

Na John Mhala,Arusha
WANAFUNZI 135,240 wa vyuo vikuu na kati hapa nchini wenye sifa stahiki na waliodahiliwa na vyuo vyao wamefanikiwa kupata mikopo ya awamu ya kwanza ya Sh Bilioni 426.5.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB), Dk Bill Kiwia mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa awamu hiyo ya kwanza ya mwaka 2025/26 yenye idadi hiyo ya wanafunzi ni wa shahada ya awali,stashahada na Samia Scholaship waliopangiwa mikopo na ruzuku.
Dk Kiwia alisema kuwa orodha hiyo ya wanafunzi 40,952 waliopangiwa mikopo ya shahada ya awali na wanafunzi 5,342 waliopangiwa mikopo ya stashahada ambapo kiasi cha Sh bilioni 152 kimetolewa.
Alisema wanafunzi 615 ni wanufaika wa ruzuku ya ‘’Samia Scholaship’’ ambao wamepangiwa ruzuku yenye thamani ya Sh bilioni 3.3 kwani wanafunzi hao ni wapya wanaojiunga na taasisi mbalimbali za elimu ya juu na kati nchini na wanafunzi 88,331 wanufaika wa mikopo wanaoendelea na masomo katika vyuo mbalimbali nchini ambao wamepangiwa mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 271.2.
Mkurugenzi huyo wa HESLB alisema kuwa hatua zinazofuata ni bodi ya mikopo kuendelea kuchakata maombi ili kupanga mikopo ya kutangaza awamu zinazofuata siku chache zijazo na hivyo kuwawezesha wanafunzi waliopangiwa mikopo kuendelea na taratibu za kuwasili na kujisajili katika vyuo walikodahiliwa.
Alisema tayari serikali imeshaipatia HESLB fedha kwa ajili ya kugharamia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na vyuo vya kati,lengo la Bodi hiyo ni kuhakikisha wanafunzi wenye sifa wanaopangiwa mikopo au ruzuku wanazikuta fedha vyuoni ambako wamedahiliwa ,kujisajili na kasha watapokea fedha ili wasome na kutimiza ndoto zao.
Mkurugenzi Dk Kiwia alisema katika bajeti ya fedha ya mwaka 2025/26 serikali imetenga shilingi bilioni 916.7 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi 273,247 kati yao wanafunzi 99,300 watakuwa ni wanufaika wa mwaka wa kwanza wa stashahada,shahada na Samia Scholaship huku wanafunzi 174,047 ni wale wanaoendelea na masomo baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka uliopita.
Alisema katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan bajeti ya mikopo ya elimu ya juu na kati imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka na katika bajeti mwaka 2024/25 kiasi cha Sh bilioni 787 kimeongezwa na serikali na kuwanufaisha wanafunzi 245,000.
Dk Kiwia ametoa ushauri kwa waombaji mikopo ya shahada ya awali,stashahada na wanufaika wa Samia Scholaship kwa mwaka huu 2025/26 watembelee SIPA-akaunti zao walizotumia kuomba mikopo au ruzuku ili kupata taarifa muhimu kuhusu maombi waliyopwasilisha HESLB ,mchakato wa upangaji wa mikopo na ufadhili wa Samia Scholaship kwa wanafunzi wenye sifa ukiendelea.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com