JMAT yasisitiza vijana kudumisha amani

MRATIBU Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) na Balozi wa Amani Taasisi ya Wanawake Nchini Korea Kusini ,Fatma Fredrick Kikkides amewataka vijana walinde amani ya nchi wasidanganyike kwa kufuata mikumbo inayofanyika kwenye mitandaoni.

Kikkides ameyasema hayo katika kipindi cha mahojiano maalumu yaliyofanyika Oktoba 23,2025 na Televisheni ya Taifa (TBC 2).

AIdha,amewataka vijana walinde amani ya nchi iliyopo wasiipoteze wao ndio nguzo kwani kundi hilo ni nguvu kazi ya Taifa.

Alifafanua vijana wanatakiwa wajitambue na kutofuata mikumbo ya wanaotaka kuharibu amani ya nchi kwa kufuata wahuni wa vijiweni wanaotaka kuharibu amani ya nchi.

“Nawaomba vijana watambue amani inaanzia kwenye nafsi, nyumbani, ofisini hivyo ni lazima muilinde amani kwa kizazi kijacho msiangalie sasa hivi tu tulipeleke Taifa la amani,”amesema Kikkides.

Aliendelea kwa kufafanua kuwa vijana wengi wana changamoto ya kukosa elimu ya kuijua amani na wengi wao kufuata makundi mabaya kwa hasira za kukosa ajira hivyo kujiingiza kwenye maamuzi ya kufuata mikumbo ya mitandaoni.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button