Mwanamke auawa kwa mapanga Mara

MARA: MWANAMKE anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40, mkazi wa Kitongoji cha Burunga, Kata ya Uwanja wa Ndege wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili. .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lumato amesema tukio hilo limetokea Oktoba 23, 2025 kati ya saa 1 na 2 usiku, na kwamba baadhi ya watu wanashikiliwa akiwemo mume wa marehemu, Wilson Charles, ambaye ni Meneja Wakala wa Barabara Vjijini na Mijini Mkoa wa Kagera.

Taarifa za awali kutoka kwa wanafamilia na majirani zinasema mauaji yalifayika chumbani kwa marehemu, ambapo kiganja cha mkono wa kulitupwa sakafuni, na mwili pembeni ya kitanda ukiwa na majeraha makubwa kifuani, mikononi, mdomoni na kwenye matiti.

Mwanafamilia Mophati Mwita ambaye alikua akimuita marehemu shangazi, alisimulia kwamba siku ya Oktoba 23 alimuagiza kijana Musa Marwa, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Serengeti aliyepanga nyumbani kwa marehemu aende kuwasha taa ya nje.

Alipotoka nje akamuona mwanaume aliyeruka ukuta kuingia ndani ya uzio, na punde akaingia mwingine, wakauliza kama mama mwenye nyumba yupo (marehemu).

“Kabla ya kujibiwa walisikia shangazi akiongea na simu, waikaingia moja kwa moja hadi chumbani. Baada ya mwanafunzi kuona hivyo akakimbilia kwa mwalimu mkuu wa shule yake kumtaarifa uvamizi huo.

“Punde nikasikia shangazi anapiga kelele lakini sikuwa uwezo wa kumsaidia kwasababu nilibaki mimi na mtoto wake ambaye ni mlemavu asiyejiweza kwa lolote. Wauaji waliondoka huku sura zao zikionekana wazi lakini sikuzitambua,” amesimulia.

Mwenyekiti wa Kitongoji, James Makuru, amesema taarifa za uvamizi alizipata kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Serengeti, na alipofika kwa marehemu akakuta tayari mauaji yameshatekelezwa.

“Niliwasiliana na Polisi, wakafika mara moja na kukagua mwili, kisha kuupeleka chumba cha kuhifadhi maiti hospitali ya wilaya.

“Na kesho yake lilionekana panga lenye damu pembeni mwa barabara, polisi wakaja kuchukua pia. Kitendo hiki ni cha kinyama hakijawahi kutokea kwenye kata yetu,” amesema.

Mkuu wa Wilaya, Anjelina Lubella, naye amethibitisha tukio hilo, akasema taarifa zaidi zitatolewa baada ya uchunguzi.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button