Copra inavyoinua wakulima mazao ya kimkakati
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imeeleza kutenga Sh bilioni nne kwa msimu wa kilimo wa 2025/2026 kwa ajili ya kununua mbegu bora za mazao matano ya kimkakati ambayo ni Mbaazi, Ufuta, Choroko, Dengu na Soya.
Awali, mazao hayo hayakupewa kipaumbele na yalikuwa yakitumika kama mboga na hata soko lake lilikuwa haliangaliwi kwa umuhimu mkubwa kama ilivyo sasa. Mkurugenzi Mtendaji wa COPRA, Irene Mlola anasema hayo wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kitaifa wa Ugawaji wa Mbegu Bora kwa Wakulima msimu wa 2025/2026 uliofanyika Shinyanga hivi karibuni.
Mlola anasema mfumo wa kidijitali umetumika kuwahudumia wakulima hao walio kwenye mnyororo wa thamani wa mazao hayo ambayo awali hayakupewa kipaumbele.
Anasema mazao hayo kwa sasa yametengenezewa mfumo madhubuti nchini na kuhakikisha yanapata masoko ndani na nje ya nchi kama mazao mengine na kwa msimu uliopita, zaidi ya tani 565,000 ya mazao mchanganyiko ziliuzwa na zaidi ya Sh trilioni moja zimekusanywa katika mfumo wa kidijitali wa ununuzi wa mazao hayo yaliyopatikana kwa wakulima waliojiunga.
SOMA: TAMISEMI, COPRA wayajenga
“Serikali imewapatia elimu ya kutosha wataalamu wa kilimo ili elimu hiyo waifikishe kwa wakulima, waweze kupata mazao ya kutosha, kwani msimu wa mwaka 2024/2025 zao la mbaazi nchini lilishika nafasi ya pili kwa mauzo nje ya nchi,” anasema Mlola.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita anasema serikali imeweka mkakati wa kuimarisha na kuinua uchumi wa nchi na wakulima kupitia mazao hayo. Anasema kwa sasa uzalishaji ni 105,000 lakini serikali iko katika juhudi za kufikia lengo la uzalishaji wa tani 127,650 ambazo ndiyo mahitaji ya sasa ya soko.
“Serikali inahakikisha wakulima wanapata mbegu bora ambazo ni msingi wa kilimo na mahitaji ya mkulima. Yote yanafanyiwa kazi ikiwa inatambua kutotosheleza kwa mbegu bora hapa nchini na mikakati inaendelea kufanyika ili mkulima aweze kunufaika,” anasema Mhita.
Anasema msimu wa 2025/2026 kuna jumla ya tani 192 za mbegu bora zilinunuliwa ambazo ni ufuta tani 126, mbaazi tani 16, choroko tani 17, dengu tani 30 na soya tani tatu zenye thamani ya Sh Bilioni 1.82.
Mhita anasema mbegu hizo zitasambazwa kwa wakulima ambao wamesajiliwa kwenye mfumo wa kupata mbegu za ruzuku na Mkoa wa Shinyanga utapatiwa tani tatu za choroko kwa msimu huo ambapo Halmashauri ya Kishapu itapata tani 1.3, Halmashauri ya Shinyanga tani 1.2 na Manispaa ya Shinyanga tani 0.5.
Mhita anawahimiza wakulima kushirikiana na maofisa ugani kutumia mbegu bora zilizothibitishwa ili kuongeza uzalishaji na mapato kwao na halmashauri.
“Wakulima msisite kupata elimu kutoka kwa wataalamu hao ili muweze kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi, kwani Mamlaka ya Hali ya Hewa imetabiri uwepo wa mvua kidogo katika msimu huu, hivyo mnao muda wa kujipanga,” anasema Mhita.
Mrajisi Msaidizi waVyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga, Kakozi Ibrahim anasema jitihada zilizofanywa na serikali kuunda mamlaka hiyo zimewasaidia kuwakutanisha na wakulima na kuwapa elimu kuhusu mfumo wa stakabadhi ghalani ambao awali walikuwa hawaukubali kwa kuona kwamba wanalazimishwa kuuza mazao yao kwa mfumo huo, wakati walilima kwa nguvu zao wenyewe.
Anasema kuwa wakulima hao wameelimika, hivyo watanufaika na wataweza kufikia malengo yao. “COPRA na TMX (Soko la Bidhaa na Mazao Tanzania) zimekuwa kitu kimoja na kuwafanya wakulima kutumia mbegu bora na kuuza kwenye soko lenye uhakika. Zamani kilimo cha mazao hayo kilikuwa cha wasiwasi, hata uuzaji wake ulikuwa holela, hongereni sana,” anasema Ibrahim.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TMX, Ian Kaduma anawapongeza COPRA kwa kusimamia vizuri ununuzi wa mazao hayo na kuahidi kuunga mkono jitihada zao ambazo wamezianzisha kwa wakulima, kuanzia hatua ya kulima hadi kuvuna na kusimamia soko.
Mwakilishi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi Ghalani (WRRB), Asangye Bangu anasema wakulima wameendelea kuelimika juu ya matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Peter Masindi anasema COPRA wamefanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanaweka mazao yao kwa pamoja na mkulima analima hapo hapo na kupata mteja ndani na nje ya nchi, ikiwa atajiunga na mfumo wa stakabadhi ghalani.
Msindi anasema COPRA imeweza kutoa somo zuri kwa wakulima. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro anasema mfumo wa stakabadhi ghalani ulianza kwa changamoto ya kulalamikiwa na wakulima na walitamani iundwe COPRA na sasa imeundwa na imekuwa ikifanya vizuri na kuwakomboa.
“Katika miaka minne, kumekuwa na mabadiliko makubwa kwenye sekta ya kilimo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekutana na watu nje ya nchi na kuunganisha masoko ya mazao, lengo ni wakulima wapate kunufaika,” anasema Mtatiro.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Mazao Mchanganyiko Manispaa ya Shinyanga, Hassan Ngoje anasema kukaa pamoja imewapa faraja, kwani watakuwa na mawazo ya pamoja tofauti na zamani walipokuwa wakilima, serikali inaonekana zaidi kwenye mavuno na kuwapangia wauze wapi bila kutoa elimu.
Akiongea kwa niaba ya wakulima wenzake, Daidus Cherehani kutoka Kijiji cha Shilabela anasema wamekuwa wakilima mazao ya choroko na dengu na kupata hasara lakini walipoanza kuuza kwa kutumia mfumo rasmi, wameanza kuiona faida.
“Tulikuwa tunauza Shilingi 800 kilogramu moja ya zao la dengu kwa wachuuzi wa mazao. Tulivyoanza kubadilika na kujiunga kwenye mfumo wa uuzaji wa stakabadhi ghalani, tumeanza kunufaika na kuuza zaidi ya Shilingi 1000 kwa kilogramu moja,” anasema Cherehani.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com