Steve Nyerere awashauri vijana uchaguzi mkuu

Msanii wa filamu na Mwenyekiti wa taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, Steve Nyerere, amewataka vijana nchini kuwa waangalifu na nyakati za sasa ambapo Serikali imejikita katika kuwaunganisha Watanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Steve aliandika ujumbe mzito akisisitiza umuhimu wa vijana kuepuka matendo yanayoweza kuhatarisha amani na mustakabali wao.

“Angalia sana maisha yako. Utulivu ni njia ya mafanikio. Yawezekana kuna vitu huvipendi, lakini kuna utaratibu wa kuvipisha na kuviweka kando ili uwe na amani ya roho,” ameandika Steve.

Ameeleza kuwa vijana wengi wamekuwa wakipotea kutokana na kufuata mkumbo, ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya na mienendo isiyo na tija, wakisahau kuwa matendo hayo ni kinyume cha sheria, afya na maadili ya jamii.

“Kufuata mkumbo kunaweza kukupoteza, ukajiona uko juu ya sheria. Kila ukiambiwa kuwa madawa ya kulevya ni haramu kwa afya yako, kwa sheria za nchi, na hata kwa utamaduni wetu unapuuzia. Sikio halisikii likishajaa ujuaji,” amesema.

Steve aliongeza kuwa ushujaa wa kweli haupo kwenye kutumia madawa ya kulevya au anasa, bali katika kujituma na kusaidia familia.

“Ushujaa wa kweli ni kusaidia familia yako, ni kupambana kutafuta riziki kwa bidii. Ukiweza kuitwa shujaa kwa sababu ya juhudi zako katika kazi na kujituma, kila mtu atakuheshimu,” ameandika.

Ametumia nafasi hiyo kuwataka vijana wa kike na wa kiume kuishi kwa kuzingatia sheria, kuepuka madawa ya kulevya na kuheshimu utulivu wa nchi, akisisitiza kuwa “hakuna aliye juu ya sheria.”

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I’m making over $25,000 a month working part-time. I kept hearing other people talk about how much money they were making online, so I decided to look into it. Well, it’s all true and has completely changed my life. This is what I do. Check it out by visiting the following link:

    COPY THIS →→→→ http://Www.Work99.Site

  2. I am making effectively tirelessly $15k to $20k basically by doing coordinate work at domestic. Multi month once more i have made $45890 from this development. astounding and smooth mac to do work and standard pay from this can be stupefying. i have propose each last one of you to connect this advance right specifically as moo security and get than full time compensation through take after this affiliation.
    :
    ) AND Great Good fortune.:
    )
    HERE====)> https://cashprofit7.site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button