Maisha yarejea kawaida, serikali yapongezwa

MAISHA ya wananchi katika mikoa yote nchini ukiwemo Mkoa wa Dar es Salaam yamerejea kama kawaida.

Wananchi kwenye mikoa mingi wameendelea kufanya shughuli zao zikiwemo za kiuchumi baada ya kuimarika kwa usalama kwenye maeneo yao.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Edward Mpogolo amepongeza vyombo vya ulinzi na usalama likiwemo Jeshi la Polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuimarisha usalama na watu kurejea katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii za kila siku.

Mpogolo amelieleza gazeti la HabariLEO kuimarika kwa usalama kumefanya shughuli za kiuchumi kuendelea kama ilivyokuwa hapo awali kwani tayari bidhaa zimeanza kuingia hususani katika masoko yaliyopo ndani ya wilaya hiyo.

SOMA: Tanzania yaihakikishia dunia usalama wa watalii

Ameonya wafanyabiashara wasiongeze bei za bidhaa zinazoingia sokoni na badala yake zibaki kuwa kama zilivyokuwa hapo awali kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria.

Mpogolo ametoa mwito kwa wananchi wa wilaya hiyo na Watanzania kwa ujumla kuwa watulivu na kufuata yale yanayoelekezwa na vyombo vya ulinzi na usalama.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume, Haji Bechina amesema Mtaa wa Karume unajumuisha masoko matatu yaliyopo kwenye wilaya hiyo likiwemo soko la Wamachinga, soko la Mtaa wa Kilwa na soko la Ilala, akiwataka wananchi wote kutoka maeneo ya nje na hapo kufika na kupata mahitaji yao kama kawaida kwani hali ni shwari.

Mfanyabishara wa Kariakoo mkoani Dar es Salaam, Ernest Henry amesema biashara katika eneo hilo zimefunguliwa na maduka mengi yapo wazi kutokana na kuimarika kwa hali ya usalama lakini wateja si wengi kama ilivyozoeleka kutokana na hofu iliyopo kwa baadhi yao pia na changamoto ya usafiri iliyoko katika baadhi ya maeneo.

Gazeti la HabariLEO lmezunguka katika baadhi ya masoko na maeneo mengine ya biashara na kushuhudia wananchi wengi Dar es salaam wamerejea katika shughuli zao za kiuchumi.

Pia, shughuli za ujenzi wa miundombinu mkoani humo ikiwemo barabara katika baadhi ya maeneo ambayo zilikuwa zimesimama kupisha kipindi cha mpito cha uchaguzi mkuu zimerudi kuendelea kama ilivyokuwa awali.

Wananchi katika maeneo mbalimbali nchini wametoa mwito wa kulinda amani.

“Tuendelee kulinda amani kwa sababu amani inapopotea hakuna shughuli yoyote inayofanyika na huduma za kijamii zinakuwa ngumu, hivyo mateso huwa mara mbili yake,” amesema mkazi wa Mbagala Rangi Tatu, Mwanahawa Issa.

Mfanyabiashara katika soko la Mkolani mkoani Mwanza, Ally Hassan amesema amepata picha halisi ya
gharama ya kukosa amani.

“Siku hiyo tulifunga maduka, biashara zikasimama, na ikumbukwe hii inatokea bila maandalizi. Baada ya hapo nikajua kuwa bila amani hakuna biashara wala maendeleo hata nchi zinazoishi bila amani siku zote zitafute namna ya kuweza kuirejesha,” alisema Hassan.

Ameongeza: “Nimepata hasara ya zaidi ya milioni saba kwenye jumla ya maduka yangu matatu, nadaiwa mkopo benki, natakiwa kulipa kodi Januari kwenye maduka yangu yote ambayo leo hii hayana kitu chochote, vyote vimeibiwa kwenye vurugu hizi… naomba serikali ituangalie japo kutuombea kusitishwa kwa riba za mikopo angalau.”

Mkazi wa Arusha, Agnes Mbaruku amesema ni vyema kuendelea kudumisha amani kwa sababu ndiyo kila kitu.
Mkazi wa Mbeya, Alison Mchunguzi alisema ni wakati wa kurejesha amani na kuendelea kuwa wamoja.

Imeandikwa na Ramla Hamidu na Prisca Pances

Habari Zifananazo

16 Comments

  1. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNANGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  2. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  3. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  4. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  5. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  6. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  7. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  8. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  9. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  10. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  11. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  12. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  13. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  14. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  15. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

  16. BAADA YA AMANI NA UTULIVU KURUDI “UNAKARIBISHWA KANISA LA 97.66% KUUNGAMA – UMETENDA MAOVU GANI, UNATAKA NINI KIBADILIKE NCHINI”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button