HESLB yatoa tuzo wanufaika mikopo

DAR ES SALAAM: Bodi ya Mikopo a Elimu ya juu (HESLB) imetoa tuzo kwa taasisi 11 zinazofanya vizuri katika kutoa taarifa za wanufaika wa mikopo hali inayoongeza kasi ya ukasanyaji mikopo.

Akizungumza wakati wa utoaji wa tuzo hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo ,Dk Billy Kawia amewapongeza taasisi hizo  zilizothibisha kwa vitendo uzingatiaji wa sheria ambapo wamekuwa mchango muhimu katika taifa kupitia uwajibikaji wao wa kuwasilisha taarifa za waajiriwa wapya na umarejesho ya mkopo kwa wakati.

“Mmechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mfuko na kuongeza uwezo wa kufikia wanafunzi wengi zaidi wanaohitaji msaada wa fedha ili kupata elimu ya juu . Nawashukuru wote walioshirikiana nasi katika utekelezaji wa sheria mmekuwa na nguzo muhimu kwa wanafunzi kujiunga elimu ya juu kila mwaka.

Ameongeza: “Leo hii kuna mtu anatuchangia karibia Sh milioni 500 kwa mwezi nawashukuru mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa mchango wenu na tuzo za le oni kutambua uzalendo wenu”.

Dk Kawia amesema tangu kuanzishwa kwa bodi mpaka leo wameshatoa kiasi  cha Sh trilioni 9.5 kwa wanafunzi wanufaika milioni 1 na ambapo kwa kila nyumba kuna mtu mmoja mkopo wa elimu ya juu umemfikia.

Amesema mwaka mwaka 2022 bodi ilikusanya Sh bilioni 169,mwaka 2023 ni Sh bilioni 177,mwaka 2024walikusanya Sh bilioni 194.5 na mwaka 2025/2026 wamefikia bilioni 220 au zaidi huku akianisha kuwa serikali ilitoa kiasi cha Sh bilioni 916.7 kwaajili ya mikopo ya elimu ya juu.

“Wakati Rais Samia anaingia madarakani tulikuwa tunapokea Sh bilioni 560  kwa mwaka huu tumepokea bilioni 916.7 na mwakani unaoanza mwezi ujao utapata kiasi cha zaidi trilioni 1 na tumeendelea kuvunja rekodi ambayo haijawahi kutokea tangu bodi kuanzishwa kwasababu wakati inaanzishwa tulikuwa tunakusanya bilioni 50 sasa tunakusanya Sh bilioni 240,”ameeleza.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..    https://www.work27.info

  2. ★彡[𝐍𝐄𝐄𝐃 𝐏𝐄𝐎𝐏𝐋𝐄 𝐅𝐎𝐑 𝐏𝐀𝐑𝐓 𝐓𝐈𝐌𝐄 𝐎𝐍𝐋𝐈𝐍𝐄 𝐖𝐎𝐑𝐊]彡★

    I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $35,000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by visiting Following Link…
    .
    You can check more……………… https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button