Mwigulu aipongezi benki udhamini Alat

DAR ES SALAAM: Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 imeendelea kuwa sehemu ya msukumo wa ushirikiano kati ya Benki ya Azania na Halmashauri nchini, unaolenga kuimarisha huduma za ukusanyaji wa mapato, ufadhili wa miradi ya maendeleo na suluhisho mbalimbali za kifedha kwa manufaa ya wananchi.

Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba, ameipongeza Benki ya Azania kwa kuwa Mdhamini Mkuu wa Mkutano Mkuu wa 40 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), unaofanyika Mwanza kuanzia Novemba 16 hadi 20, 2026.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania, Yahaya Mbanka, akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dk. Esther Mang’enya, amesema udhamini huo unaonesha dhamira ya benki kuimarisha ushirikiano na halmashauri nchini.

“Mafanikio ya ushirikiano huu hayatapimwa kwa ukubwa wa udhamini, bali kwa matokeo yatakayopatikana katika maendeleo ya Halmashauri na maisha ya wananchi,” amesema Mbanka.

Habari Zifananazo

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button