Gabriel Jesus amerejea!

LONDON: MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Gabriel Jesus, amerejea mazoezini baada ya kukosekana uwanjani kwa miezi 10 kutokana na majeraha aliyoyapata mwezi Januari katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Manchester United.
Katika ‘video’ fupi zilizowekwa jana jioni na timu hiyo kwenye mtandao wa Instagram, zilimuonesha Jesus akiwa mazoezini na kikosi cha kwanza cha timu hiyo akifanya mazoezi.
Jesus alinukuliwa akisema: “Ndiyo, najisikia vizuri. Goti langu linapona vizuri sana. Kwa hivyo natarajia kuwa karibu na timu hivi karibuni, kurudi kufanya kile ninachopenda kufanya. Imekuwa muda mrefu sana”.
Baada ya kurejea nyota huyo, Arsenal wanamatumaini ya kurejea kwa Martin Odegaard, Noni Madueke, Kai Havertz Martin Zubimendi, Viktor Gyokeres katika mchezo wa dabi dhidi ya Tottenham Hotspurs baada ya mechi za FIFA.



