Wizara ya Nishati yatoa elimu nishati safi Mbeya

MBEYA: Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Simon Parmet, ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kutoa elimu kwa Maofisa Dawati kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Hatua hiyo imeelezwa itachochea kasi ya utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia na kusaidia kufikia lengo la Serikali la kuwa na asilimia 80 ya Watanzania wanaotumia nishati safi ifikapo mwaka 2034.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya maofisa wanaoratibu utekelezaji wa mkakati huo kwa mikoa na Halmashauri za Nyanda za Juu Kusini, yaliyofanyika mkoani Mbeya, Parmet alisema elimu hiyo imekuja kwa wakati muafaka kwani mikoa hiyo inaongoza kwa kilimo na uzalishaji wa mazao ya miti, lakini bado matumizi ya kuni na mkaa ni makubwa.

“Mikoa hii inaongoza kwa kilimo cha miti, lakini pia matumizi ya kuni ni makubwa. Elimu hii itasaidia Maofisa Dawati kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia na kuachana na mapishi ya mazoea,” alisema Parmet.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia kutoka Wizara ya Nishati, Benezeth Kabunduguru, alisema mafunzo hayo ni endelevu na yanalenga kuhakikisha kila Ofisa Dawati nchini anapata uelewa wa kina kuhusu nishati safi ya kupikia, ili waweze kuwafikia wananchi kwa urahisi na ufanisi zaidi.
“Tunataka kila Afisa Dawati awe na uelewa wa kina kuhusu nishati safi ya kupikia ili aweze kuwafikia wananchi kwa ufanisi. Lengo letu ni kufikia asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi ifikapo mwaka 2034,” alisisitiza Kabunduguru.

Ameongeza kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia ni kipaumbele cha taifa na dunia kwa ujumla, kutokana na mchango wake katika kulinda mazingira, kuboresha afya za wananchi na kuinua uchumi wa kaya.
Naye, Ofisa Mwandamizi Mshauri Masuala ya Kiufundi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Deusdedit Malulu, aliwahimiza Maofisa Dawati kutumia mafunzo hayo kutangaza fursa za uwekezaji na ujasiriamali katika sekta ya nishati safi ya kupikia, ikiwemo utengenezaji wa majiko banifu, mkaa mbadala, na miradi ya ruzuku kupitia REA.

“Tunataka kuona maafisa wakitumia mafunzo haya kuhamasisha vijana na vikundi vya wajasiriamali kuanzisha miradi ya nishati safi itakayowanufaisha kiuchumi,” alisema Mhandisi Malulu.
Mafunzo hayo yamehusisha Maafisa Dawati wa Halmashauri na Mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Katavi, Rukwa, Njombe na Ruvuma.




Nchi ya Syria ndio inaongoza kuwa na watu wengi chini ya himaya ya UNHCR ambako kuna jumla ya wakimbizi milioni 6.8, nchi inayofuata ni Venezuela ambayo ina jumla ya wakimbizi milioni 4.9.
Nchi nyingine mbili ni Afghanistan inayoshika nafasi ya tatu kwakuwa na idadi ya wakimbizi milioni 2.8 ikifuatiwa na taifa changa zaidi Afrika, nchi ya Sudan Kusini ambayo ina jumla ya wakimbizi milioni 2.2. Myanmara inashika nafasi ya 5 ikiwa na wakimbilizi Milioni 1.1 wanaosimamiwa na shirika hili la Umoja wa Mataifa
Na nchi inayoongoza kukaliwa na wakimbizi wengi ni Uturuki, ambayo imekaribisha takriban wakimbizi milioni 4, wengi wa wakimbizi hawa ni raia wa Syria ambao ni sawa na asilimia 92 ya wakimbizi wote nchini humo.
Nchi ya Colombia, taifa hili linahifadhi wakimbizi kutoka nchi mbalimbali lakini wanaoongoza kwa idadi kumbwa ni Venezuela ambao wako zaidi ya milioni 1.7.
Ujerumani inashika nafasi ya tatu duniani kwakuwa na idadi kubwa ya wakimbizi ambako takwimu zinaonesha jumla yao ni takriban milioni 1.5, katika nchi hii pia raia wa Syria pamoja na waomba hifadhi wanafikia asilimia 44 ya wakimbizi wote.
Mataifa yanayoshika namba 4 na 5 ni Pakistan na Uganda ambayo yamehifadhi jumla ya wakimbizi milioni 1.4 kila moja.
Takriban watoto milioni moja wamezaliwa nje ya mataifa yao kati ya mwaka 2018 na 2020, idadi hii ni sawa na uwiano wa watoto kati ya 290,000 na 340,000 kwa mwaka.
Watoto hawa wapo kwneye hatari ya kuendelea kuishi uhamishoni kwa miaka mingi zaidi na wengine maisha yao yote bila kurejea kwenye taifa lao la Venezuela.
Pamoja na kuwa wakimbizi wanakuwa wa rika zote lakini takwimu za UNHCR zinaonesha watoto wamechukua asilimia 30 ya wakimbizi wote duniani.
Kwakutazama uwiano wa mabara, nchi tatu za Kusini mwa jangwa la Sahara ndio zinazo ongoza kuwa na idadi kubwa ya wakimbizi watoto.
Afrika Magharibi na Jamhuri ya Afrika ya Kati zina idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wanawake na wasichana ambao jumla yake ni asilimia 54 zaidi ya nchi nyingine yeyote.
Mgogoro wa wakimbizi wa Ukraine ulianza na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo Februari 2022. Kufikia Septemba 2025, UNHCR imerekodi wakimbizi wa Kiukreni milioni 5.7 kote ulimwenguni, huku 90% ya idadi hii wakiishi katika nchi mbalimbali za Ulaya nje ya Ukrainia
Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting websiteMore Details For Us→→ http://www.job40.media