Arusha kuandaa mkutano wa kwanza wa AI Afrika

ARUSHA: Jiji la Arusha linajiandaa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Afrika wa Akili Mnemba (Africa Premier AI Conference – APAIC 2025) utakaofanyika kuanzia Novemba 24 hadi 27, 2025, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Akizungumza kuhusu maandalizi hayo, Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa APAIC 2025, Abdulwahid Ali Khamis, alisema mkutano huo utalenga kujadili na kuweka mikakati ya maendeleo ya Akili Mnemba (AI) barani Afrika chini ya kauli mbiu “Kuchambua Agentic AI kwa Mageuzi ya Kijamii na Kiuchumi Barani Afrika.”

“Zaidi ya wajumbe 1,200, wazungumzaji 150, na washiriki kutoka zaidi ya nchi 40 wanatarajiwa kuhudhuria. Tofauti na makongamano mengine, APAIC 2025 italenga zaidi utekelezaji wa ubia kati ya serikali, sekta binafsi, wawekezaji na wabunifu ili kutumia AI kuboresha afya, elimu, kilimo, biashara na utawala bora,” alisema Khamis.

“Mkutano huo unaandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Elimu na Sayansi na Teknolojia na COSTECH.

Miongoni mwa matukio muhimu katika mkutano huo ni uzinduzi wa The Dawn Directive mfumo wa kwanza wa uelewa na umahiri wa AI duniani, pamoja na Azimio la Mombasa kuhusu Agentic AI, litakaloweka dira ya Afrika kuhusu maadili, uwajibikaji na usimamizi wa teknolojia hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mkutano, Anthony Nivo, alisema kuchaguliwa kwa Arusha kuwa mwenyeji wa APAIC 2025 ni uthibitisho wa nafasi ya Afrika Mashariki katika mapinduzi ya kidijitali.

“AI si teknolojia ya kesho ni ya leo. Kuandaa APAIC 2025 hapa Arusha ni hatua ya kihistoria katika kuamua jinsi Afrika itakavyonufaika na mapinduzi ya akili mnemba,” alisema Nivo.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting websiteMore Details For Us→→ http://www.job40.media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button