Kutangazwa mshindi hadi kuapishwa Rais wa Tanzania
NOVEMBA Mosi mwaka huu ndani ya ukumbi wa makao makuu ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jacobs Mwambegele anatangaza matokeo ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Kwa sauti thabiti, Jaji Mwambegele anatamka jina lililosubiriwa kwa hamu na Watanzania wengi.
Anasema, “Kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, ikisomwa pamoja na Kifungu cha 45 (9) (10) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Namba 1 ya Mwaka 2024 na Kanuni ya 57 (C) ya Kanuni za Uchaguzi za Mwaka 2025, ninamtangaza Samia Suluhu Hassan kuwa Rais Mteule kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.”
Aidha, anamtangaza Dk Emmanuel Nchimbi aliyekuwa mgombea mwenza wa CCM kuwa Makamu wa Rais Mteule, kwa mujibu wa mamlaka yaliyotajwa katika Ibara ya 47(2) ya Katiba, ikisomwa pamoja na Kifungu cha 47 cha sheria hiyo hiyo.
Anatangaza mbele ya wawakilishi wa vyama vya siasa, asasi za kiraia, vyombo vya habari na waangalizi wa ndani na wa kimataifa katika makao makuu ya INEC jijini Dodoma. Samia Suluhu Hassan; mgombea wa CCM alipata ushindi huo baada ya kujikusanyia kura milioni 31.9 sawa na asilimia 97.66 ya kura halali 32,678,844 zilizopigwa. Katika uchaguzi huo kura zilizoharibika zilikuwa 124,466, sawa na asilimia 0.38.
Wingi wa kura ulithibitisha ushindi wa kihistoria uliomfanya Samia kuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa Rais kupitia sanduku la kura katika historia ya Tanzania. Kabla ya tangazo hilo, Mwambegele anasema wapigakura waliosajiliwa walikuwa 37,647,255, huku 32,803,310 wakijitokeza kupiga kura, sawa na asilimia 86.8 ya waliojiandikisha.
Kisha, Jaji Mwambegele anakabidhi vyeti vya ushindi kwa Samia kama mteule wa kiti cha rais na Dk Emmanuel Nchimbi kama mteule wa kiti cha makamu wa rais. “Matokeo hayo ni ya mwisho na hayawezi kupingwa mahakamani, kwa mujibu wa Katiba,” anasema Jaji Mwambegele.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi, Samia anasema: “Ninawashukuru wananchi kwa imani yenu na kwa heshima kubwa mliyonipa kwa kunichagua kubeba tena dhamana hii kubwa ya kuliongoza taifa letu.” “Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia mimi tumepokea cheti cha ushindi cha uchaguzi mkuu kwa heshima na unyenyekevu mkubwa sana,” anasema.
Anaongeza: “Cheti hiki ni uthibitisho wa imani ya wananchi kunikabidhi mimi na Chama Cha Mapinduzi dhamana ya kwenda kutekeleza ahadi yetu ya kuimarisha, kulinda na kujenga heshima na utu wa Mtanzania.” Anaongeza: “Kila kura iliyopigwa ilikuwa na umuhimu wake na kila kura imetuma ujumbe wa maoni kwa serikali tutakayoiunda.”
Samia anaahidi kutekeleza kikamilifu ahadi zote zilizomo katika Ilani ya CCM, akisisitiza kwamba serikali yake itazingatia umoja, ustawi na maendeleo jumuishi.
“Wananchi wamechagua ‘Kazi na Utu’ na wamechagua kusonga mbele, ahadi yetu mimi na mwenzangu makamu wa rais mteule ni kwamba, tunakwenda kufanya kile tulichoahidi kwenye ilani na yale yote tutakayoona yanafaa kwa nchi yetu, tunasema asanteni sana Watanzania wote.”
Samia anatumia fursa hiyo kupongeza wagombea wenzake 16 kwa kuendesha kampeni zenye ustaarabu na zilizokijikita kwenye hoja.
“Mmeendesha kampeni safi na kiistarabu, mawazo yenu yamekuwa sehemu muhimu ya mjadala wetu wa kisiasa na yameimarisha ari ya kuelekeza siasa zetu kwenye masuala ya maendeleo. Ninawashukuru wagombea wote walioridhishwa na kazi yote iliyosimamiwa na Tume na kukubali matokeo.”
Anasema uchaguzi ulikuwa wa kihistoria kutokana na kugharamiwa na rasilimali za ndani, na ni mara ya kwanza kuwa na wagombea wanawake watatu walijitokeza kuwania urais na huku kukiwa na idadi kubwa ya wanawake waliojitokeza kwa nafasi ya mgombea mwenza.
“Tume imeonesha ukomavu mkubwa kwa kutoa fursa sawa kwa vyama vyote,” anasema Samia, akisisitiza kuwa demokrasia ya Tanzania imepiga hatua kubwa. Aidha, anahimiza Watanzania kuungana na kusahau tofauti za kisiasa. “Tujenge madaraja yanayotuunganisha, si kuta zinazotutenganisha. Tanzania ni yetu sote,” anasema.
Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ikiongozwa na Makamu wa Rais wa zamani wa Uganda, Dk Specioza Kazibwe inatoa tathmini chanya kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi. Anasema katika Uchaguzi Mkuu wa 2025, Tanzania imeonesha ukomavu wa kisiasa na mfano bora wa kuigwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.
“Sijawahi kuona hili sehemu nyingine wagombea wote kukaa pamoja muda mfupi baada ya uchaguzi na kukubali matokeo. Mwishowe, Tanzania ndiye mshindi wa kweli,” anaeleza. Anaongeza: “Tulipofika tulikuta Tanzania yenye
amani, na tunapoondoka tunaiacha Tanzania yenye amani.”
Kwa niaba ya wagombea wote, Almas Hassan Kisabya wa NRA anasema, “Tumeridhika na matokeo kwa sababu yanaonesha uamuzi halali wa Watanzania. Huu si ushindi wa chama, bali ushindi wa taifa.”
Wagombea hao waliahidi kushirikiana na serikali mpya kujenga taifa lenye umoja na maendeleo, huku wakiahidi kutumia majukwaa yao ya kisiasa kutoa elimu ya uraia na amani.
Hatua ya mwisho ya safari hiyo ya kihistoria ilikuwa sherehe ya kuapishwa kwa Rais Mteule zilizofanyika Novemba 3 mwaka huu zilizofanyika katika Uwanja wa Nishani katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma ikiwa ni siku mbili baada ya kutangazwa mshindi.
Eneo la kuapishia lilikuwa limepambwa kwa rangi za taifa ambazo ni kijani, njano, na nyeusi sambamba na gwaride maalumu la kijeshi ikiwa ni ishara ya heshima kwa Rais mpya wa Tanzania. Baada ya kuapishwa Wimbo wa Taifa uliimbwa kuashiria mwanzo mpya wa safari ya maendeleo.
Baada ya kiapo, Samia anatoa mwito kwa Watanzania kuepuka mihemko, vurugu, chuki na kugawanyika. “Nimepewa dhamana ya kuwa mtumishi mkuu wa taifa katika kuwaletea maendeleo endelevu kwa maana ya uimara wa kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia na kijamii,” anasema.
“Niwasihi Watanzania tuchague hekima badala ya ghadhabu, busara badala ya mihemko, upendo badala ya chuki, uvumilivu badala ya vinyongo, umoja badala ya mgawanyiko, amani badala ya vurugu, unyenyekevu badala ya kiburi na huruma badala ya hasira, taifa letu ni bora na lina nguvu zaidi kuliko mtu yeyote,” anasisitiza.
Oktoba 29, 2025 Tanzania ilifanya Uchaguzi Mkuu wa Saba katika Mfumo wa Siasa wa vyama vingi na Samia Suluhu Hassan akaibuka kuwa mshindi wa kiti cha urais huku Dk Nchimbi akiwa makamu wa rais. Uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo huo ulifanyika mwaka 1995, ambapo Benjamin Mkapa alimshinda Augustine Mrema, na kisha akarejea madarakani mwaka 2000.
Mwaka 2005, Mkapa alikabidhi madaraka kwa Jakaya Kikwete ambaye alihudumu kwa miaka 10 kabla ya Dk John Magufuli kuchaguliwa mwaka 2015. Kufuatia kifo cha Magufuli mwaka 2021, aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo, Samia alipokea jukumu la kuiongoza nchi kwa nafasi ya urais na kumteua Dk Philip Mpango kuwa Makamu wake.
Uchaguzi wa mwaka huu sasa unamuidhinisha rasmi Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa kwanza mwanamke aliyechaguliwa kwa kupigiwa kura na wananchi katika historia ya Tanzania.




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com
I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…
Try it, you won’t regret it!….. https://www.job40.media