Huduma mpya TTCL kukuza uchumi kidijitali

DAR ES SALAAM: SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linaendelea kukuza uchumi wa kidijitali kwa kuhakikisha inatoa huduma bora kwa gharama nafuu.
Agenda hiyo ambayo pia inaungwa mkono na serikali inakuja baada ya kampuni hiyo kuzindua huduma mpya ya kisasa ya T-Fibre Triple Hub kifurushi kipya chenye huduma tatu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Promosheni wa TTCL, Janeth Maeda, amesema kifurushi hicho ni sehemu ya jitihada za shirika hilo kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora, za uhakika na kwa gharama nafuu, sambamba na kuunga mkono ajenda ya serikali ya kukuza uchumi wa kidijitali.
Huduma hii ya “Faiba Mlangoni Kwako – T-Fibre Triple Hub” inajumuisha huduma tatu kuu ambazo ni: Intaneti ya kasi bila kikomo (Unlimited Internet) kwa matumizi ya nyumbani, ofisini au kwenye biashara; Huduma ya Simu ya Mezani (Landline Voice Service) kwa ajili ya mawasiliano ya moja kwa moja kupitia mtandao wa faiba; na Huduma ya Intaneti na Dakika kwa Simu ya Mkononi (Mobile Services) inayomwezesha mteja kutumia laini ya TTCL kupata GB na dakika kwa matumizi popote alipo.

Kwa mujibu wa Maeda, kifurushi hiko kimeundwa kwa kuzingatia mahitaji ya kizazi cha sasa cha kidijitali kinachohitaji huduma bora, rahisi kutumia na zenye thamani halisi kwa gharama nafuu. Alisema kuwa huduma hizo zinapatikana kwa bili moja tu kwa mwezi, jambo linalorahisisha maisha ya wateja na kupunguza gharama za uendeshaji wa huduma nyingi tofauti.

Kifurushi cha T-Fibre Triple Hub kinapatikana kuanzia Sh 70,000 kwa mwezi, na mteja atapata Intaneti ya kasi ya hadi 20 Mbps kwa kupakua na kupakia, dakika 300 za mawasiliano, pamoja na GB 20 za intaneti kwa simu ya mkononi.
TTCL imeeleza kuwa huduma hii inalenga kufika hadi katika makazi ya watu, taasisi, na wafanyabiashara, ili kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na huduma za kisasa za mawasiliano, bila kujali eneo analoishi.
Kwa uzinduzi huu, TTCL imeandika historia kuwa shirika la kwanza nchini kutoa kifurushi kinachojumuisha huduma tatu kwa pamoja, hatua inayoonyesha dhamira yake ya kuendelea kuwekeza katika teknolojia na ubunifu wa kidijitali.

Maeda alihitimisha kwa kusema kuwa TTCL itaendelea kusikiliza maoni na mahitaji ya Watanzania ili kuboresha huduma zake na kuhakikisha kila nyumba, kila ofisi na kila biashara inapata mawasiliano ya uhakika, yakichochea maendeleo na kuimarisha uchumi wa kidijitali wa taifa.




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com