Kikongwe wa miaka 93 aomba Serikali kumlinda

KIKONGWE mwenye umri wa miaka 93, Eliashisauwa Isay, mjane wa kijiji cha Ngira, kata ya Masama Mashariki wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, amemuomba serikali kuingilia kati mgogoro unaomhusisha na mkwewe anayedai nyumba yake.

Mama Isay amesema anaishi kwa hofu kubwa baada ya nyumba yake kuchomwa moto na watu wasiojulikana mnamo Oktoba 24, mwaka huu, majira ya asubuhi. “Tuliamka kama kawaida kuendelea na shughuli za kila siku, ghafla tukaona moshi mkubwa ukitoka sebuleni. Tulipochungulia, tukagundua nyumba inaungua,” alisema kwa uchungu mjane huyo.

Binti yake wa mwisho, Caroline Isay, amesema baada ya kuona moshi waliita majirani kwa msaada. Walijitokeza kwa wingi, wakiwemo mwenyekiti wa kijiji, Daudi Muro, na kusaidia kuzima moto huo. Muro aliongeza kuwa baada ya tukio hilo alikagua na polisi, lakini chanzo cha moto hakikubainika mara moja.

Kikongwe huyo amesema tangu kufariki kwa mwanawe Fred, ambaye alikuwa mume wa mkwe anayesemekana kutoa vitisho, amekuwa akipokea maneno ya kumtaka aondoke nyumbani.“Nyumba hii ilijengwa na marehemu mume wangu miaka ya 1980. Hapa ndipo nilipozalia watoto wangu nane, watano kati yao tayari wamefariki, akiwemo Fred. Baada ya kifo chake, mkwe wangu alianza kudai nyumba hii ni yake, akasema mimi niende mahali pengine. Hili halina ukweli hata kidogo,” alisema mama Isay.

Ameeleza kuwa anaishi kwa wasiwasi mkubwa na anaogopa tukio la kuchomwa nyumba lilihusiana na mgogoro huo wa familia. “Sina pa kwenda, naomba serikali inisaidie. Siwezi kutoka kwenye nyumba hii ambayo mume wangu alijenga kwa mikono yake,” aliongeza kwa huzuni.

Baadhi ya majirani, ambao ni wakongwe, wamesema wanaufahamu vyema ujenzi wa nyumba hiyo tangu ulipoanza hadi kukamilika, wakithibitisha kuwa nyumba hiyo ilijengwa na marehemu Isay. “Tuliuona ujenzi huu tangu mwanzo. Nyumba hii ni mali ya wazazi hao, si kweli kwamba ni ya mkwe na tunashangaa kuona anataka kumhamisha,” alisema Jamila Silvanus, mmoja wa majirani.

Mama Isay sasa anaiomba serikali na viongozi wa dini kuingilia kati mzozo huo, akisisitiza kuwa anahitaji tu amani katika siku zake za uzee. SOMA: Chalamila arudisha tabasamu kwa Alice

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I have just received my 3rd payment order and $30,000 that I have built up on my laptop in a month through an online agent…!v76) This job is good and his regular salary is much better than my normal job. Work now and start making money online yourself.
    Go here….… https://Www.Smartpay1.site

  2. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  3. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button