Mwigulu aapishwa kuwa Waziri Mkuu

DODOMA: RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 14, amemuapisha Waziri Mkuu mteule, Dk. Mwigulu Nchemba, kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza katika hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Rais Samia amesema uteuzi huo umezingatia mambo mbalimbali yaliyochunguzwa kwa maslahi ya taifa.
Rais Samia alimuagiza Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, ili ahadi zilizotolewa kwa wananchi zitekelezwe kama ilivyopangwa.
Aidha, Rais Samia alimuonya Waziri Mkuu Dk. Mwigulu kuwa muangalifu na vishawishi vinavyoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa majukumu yake, akibainisha kwamba cheo hicho kimebeba majukumu makubwa ya taifa na hakina undugu, familia au urafiki. “ Sijui Majaliwa alivyochaguliwa alikuwa na miaka mingapi, lakini wewe unapaswa kuwa makini sana,” alisema Rais Samia.
Hafla ya uapisho imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi wa siasa, viongozi wa dini na wengine. SOMA: Bunge lamthibitisha Mwigulu



