Rais Mwinyi ashuhudia uapisho wa Mwigulu

DODOMA: RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameshiriki hafla ya uapisho wa Waziri Mkuu mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba, ambaye ameapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Samia Suluhu Hassan. Hafla hiyo imefanyika leo Novemba 14, 2025, Ikulu ya Chamwino.

Dk. Mwigulu aliteuliwa hivi karibuni baada ya kupendekezwa na Rais Samia na kupigiwa kura na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano jana Novemba 13, 2025. Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Emmanuel Nchimbi, viongozi wa Serikali wastaafu na waliopo madarakani kutoka SMT na SMZ, Wabunge, viongozi wa vyama vya siasa, vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini na wageni waalikwa.

Rais Dk. Mwinyi amewasili leo Dodoma kutoka Zanzibar kuhudhuria hafla hiyo pamoja na Uzinduzi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. SOMA: Mwigulu aapishwa kuwa Waziri Mkuu

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button