TAKUKURU, Comoro kushirikiana mambo matano
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema Tanzania na Comoro zitaendelea kushirikiana katika maeneo matano ikiwemo utawala bora.
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Chrispin Chalamila amesema hayo alipotembelewa na ugeni kutoka Comoro
ulioongozwa na Rais wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya nchi hiyo, Fahamoue Youssouf.
Chalamila amesema ushirikiano kati ya Comoro na Tanzania umejengwa katika misingi ya kuheshimiana, kuunganishwa na tamaduni za kila nchi pamoja na kuwa na malengo ya pamoja ya amani na maendeleo.
“Kwa miaka kadhaa tumekuwa tukishuhudia maeneo kadhaa yakiimarika, hususani katika maeneo ya utawala bora na jitihada za kuzuia na kupambana na rushwa. Ushirikiano huu umekuwa ukifanyika kupitia ushirikiano wa kikanda pamoja ushauri wa Bodi ya Ushauri ya Umoja wa Afrika dhidi ya Rushwa (AUABC),” alisema Chalamila.
Amesema eneo jingine ni kubadilishana uzoefu kuhusu hatua za kupunguza rushwa na kushirikiana katika kuimarisha mifumo ya kitaifa ya kiuadilifu, nyenzo za kutafuta vihatarishi vya uwepo wa rushwa na utekelezaji wa mapendekezo yanayotolewa na wadau ili kuziba mianya ya rushwa.
Amesema eneo lingine la ushirikiano ni usalama na utekelezaji wa sheria kupitia juhudi za pamoja katika kuimarisha na kusimamia mipaka, hasa usalama wa Bahari ya Hindi pamoja na bandari, kwa kutumia fursa za miundombinu ya Tanzania na muunganiko na Comoro ili kuweka mipango ya kukuza biashara, utalii na uwekezaji.
Amesema eneo la nne ni kilimo, mafunzo na kujengeana uwezo kupitia programu mbalimbali za kubadilishana uzoefu na mafunzo kwa watumishi wa umma na katika utawala na uongozi.
“Kumekuwa na ushirikiano katika taratibu za utoaji wa ufadhili wa masomo na ushirikiano wa taasisi za elimu ya juu kati ya nchi hizi, na tutaendelea kuimarisha ushirikiano wetu kwa manufaa ya nchi zetu,” alisema Chalamila.
Alitaja eneo jingine la ushirikiano kuwa ni sekta ya afya na maendeleo ya jamii, kwa kupambana na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na kuimarisha mifumo ya afya ya umma kwa ujumla.
Chalamila alisema kwa sasa taasisi hiyo ina jumla ya ofisi 145 ambazo ni makao makuu, 28 za mikoa, 111 za wilaya pamoja na vituo maalumu sita katika maeneo yenye mzunguko mkubwa wa fedha na mipakani.
Rais wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Comoro, Youssouf alisema ujio wao unaonesha uwazi wa taasisi hizo kupitia suala la kubadilishana uwezo juu ya mapambano ya rushwa kikanda na Afrika kwa ujumla.
Alisema ushirikiano huo utafungua njia ya ushirikiano endelevu, iwe kupitia mafunzo, uzoefu au kuanzishwa kwa mifumo rasmi kati ya nchi hizo.
Aliongeza kuwa matarajio yao ni kuhakikisha azimio la pamoja linatimia kwa kuwa watajifunza kutokana na uzoefu na matarajio yenye matumaini ya ushirikiano kati ya taasisi hizo kwa lengo la kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com