Nchi EAC ziondokane vikwazo vya kibiashara

MAONESHO ya 25 ya Biashara Ndogondogo na za Kati (MSMEs) yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Jiji la Nairobi nchini Kenya yamedhihirisha umuhimu wa kuachana na vikwazo vya kibiashara kwani havina kitu zaidi ya kukwamisha biashara za Afrika Mashariki.

Ukuaji wa kibiashara na uwekezaji ni ndoto na shabaha ya Sekretarieti ya Afrika Mashariki kwani ndiyo nyenzo pekee inayowezesha ukuaji wa kiuchumi kwa nchi moja moja na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Hili halitawezekana ikiwa nchi hizo zitaendelea kukumbatia vikwazo vya kibiashara kwa visingizio kuwa zinalinda biashara na wazalishaji wa ndani kwa sababu hata huo uzalishaji wa ndani unahitaji soko kubwa la EAC kwa ajili ya kuuza bidhaa zao.

SOMA: Maonesho Juakali EAC yakonga mawaziri Tanzania, Uganda

Ufunguzi wa maonesho hayo ulishuhudia wafanyabiashara kutoka Afrika Mashariki wakionesha uvumbuzi na bunifu zao mbalimbali pamoja na ushirikiano wao kibiashara.

Wakati wa kufunga maonesho hayo, Rais Dk William Ruto alikemea dhana ya uwekaji wa vikwazo mipakani kwa manufaa ya nchi moja wakati malengo ya kuunganisha mataifa ya EAC ni kuileta faida kwa mataifa yote kwa kuruhusu biashara za kuvuka mipaka.

Tunaungana na Rais Ruto kukemea vizuizi vya kibiashara kwa sababu havina malengo ya kukuza muungano wa EAC, badala yake vinaleta mpasuko baina ya nchi wanachama kinyume na sheria na mkataba wa EAC.

Mathalani, hata biashara ya ndani ya EAC kukua kwa asilimia 27, kutoka Dola bilioni 14.2 hadi Dola bilioni 18 kati ya Juni 2024 na Juni 2025, ni kutokana na milango ya biashara kufunguliwa kati ya mipaka ya nchi na nchi.

Laiti kama milango ingefungwa kwa kuwekwa vikwazo, leo tusingeweza kueleza namna biashara ya EAC ilivyoongezeka kwa asilimia 22 na kupanda kutoka Dola bilioni 115.4 hadi Dola bilioni 140.8 nje ya EAC.

Ni rai yetu kwa Sekretarieti ya Afrika Mashariki kushirikiana na nchi wanachama kuhakikisha vikwazo vya kibiashara vinakomeshwa.

Ni ukweli kuwa kuongezeka kwa biashara ya kikanda na uwekezaji kunaonyesha kukomaa kwa soko la ndani, ambalo linazidi kufafanuliwa na ubunifu, ushindani na dhamira ya pamoja ya wananchi wa Afrika Mashariki kufanya biashara zaidi baina yao na kufanikiwa pamoja.

Tunaamini kuwa maonesho hayo yanatoa wakati muhimu wa kukabiliana na masuala yanayotatiza biashara kabla ya mkutano ujao wa wakuu wa EAC uliopangwa Desemba 2025.

Ni kawaida kuwa kupitia maonesho, warsha na ushirikiano kati ya biashara na biashara, washiriki hupata ujuzi mpya, kuchunguza teknolojia zinazoibuka na kuimarisha ushindani wao ndani na nje ya eneo hili.

Ili kupanua soko la EAC, nchi wanachama zinatakiwa kuimarisha uzalishaji wa ndani, kuongeza mnyororo wa thamani wa kikanda na kuimarisha upatikanaji wa fedha, teknolojia na masoko.

Tunahimiza nchi wanachama kutekeleza kikamilifu mkataba wa EAC kwa kuruhusu biashara za kuvuka mipaka ili mradi sheria na taratibu za nchi husika zifuatwe.

Habari Zifananazo

4 Comments

    1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
      .
      HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

    2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button