Dk Kijaji: Tutajali utu wa kila mtu

DODOMA: Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Ashatu Kijaji amewataka watumishi wa wizara na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kuzingatia maslahi na utu wa Mtanzania wanapotoa huduma kwa wananchi.
Dk Kijaji ametoa maelekezo hayo jana November 18 akiwa jijini Dodoma mara baada ya kuripoti kazini na kufanya mazungumzo na menejimenti ya wizara, muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Amesema ni muhimu watumishi kufanya kazi kwa kuzingatia utu na maslahi ya wananchi ili kuhakikisha wanapata huduma bora na maendeleo wanayostahili.
“Wananchi wanatuhitaji kwa yale tuliyoaminiwa kuyatekeleza kwa niaba ya Watanzania milioni 61. Ni jukumu letu kuwawezesha ili waendelee kuishi vizuri kama kawaida,” amesema Dk Kijaji.

Amefafanua kuwa Ilani ya CCM imeweka mkazo katika ustawi wa watu, na ustawi huo hauwezi kupatikana endapo changamoto kama wanyamapori waharibifu hazitatatuliwa.
“Mkulima amelima ekari 20 za mbaazi, zimekomaa, halafu zinaharibiwa na tembo, ustawi haupo hapo. Hivyo lazima tufikirie mbali ili kulinda ustawi wao,” amesisitiza.

Ameongeza kuwa falsafa ya Kazi na Utu ya Mhe. Rais inahitaji mtumishi kumweka mwananchi mbele: “unapomhudumia mtu, jiulize ungependa kuhudumiwa vivyo hivyo? Huo ndio msingi wa kazi yetu.” amesema Dk Kijaji.
Waziri Kijaji pia ametoa wito kwa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na mshikamano ili kutimiza ndoto za Watanzania kupitia sekta za uhifadhi, maliasili na utalii.

Aidha, amewapongeza kwa kazi wanayoifanya na kuhimiza kuendeleza ushirikiano ili kufikia malengo ya wizara.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Hamad Hassan Chande ameishukuru menejimenti na watumishi kwa mapokezi mazuri na kusisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa kuzingatia utu.
“Tumekuja kuungana nanyi katika ujenzi wa taifa. Hatukuja kama watawala, bali kama viongozi wa kutimiza ndoto ya Rais fanyeni kazi kwa utu, na mtambue thamani ya watu,” amesema Chande.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Hassan Abbas, ameahidi kutoa ushirikiano kwa uongozi mpya ili kufanikisha malengo ya wizara na serikali, hususan katika kuhudumia wananchi na kutangaza vivutio vya utalii.
Awali, Waziri Dk. Kijaji alikagua gwaride maalum lililoandaliwa na Jeshi la Uhifadhi (JU) akiongozwa na Katibu Mkuu, Dk. Abbas.




Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us →→→→→→→ https://Www.Work27.Online
I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com