NEMC yashiriki UNFCCC COP-30

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki Mkutano wa thelathini wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC COP-30), unaoendelea jijini Bélem, Brazil unaotarajiwa kukamilika Novemba 21, 2025.
Akiongoza ujumbe wa NEMC katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyeambatana pia na Makamu Mwenyekiti, Wakili Alex Mgongolwa amewataka watumishi wa Baraza kuhakikisha wanatumia vyema jukwaa la mkutano huo kupata fursa za fedha za miradi ili kuweza kuhakikisha unaleta matokeo chanya katika kutekeleza vyema nguzo ya mazingira katika Dira ya Taifa ya 2050.

Katika kutekeleza hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dk Immaculate Sware Semesi, ameongoza ujumbe wa NEMC kwenye mikutano mbalimbali ya uwili ili kuimarisha ushirikiano na wadau katika sekta ya Mazingira.
Baadhi ya Mikutano hiyo ni pamoja na mkutano wa uwili na Benki ya Maendeleo ya Africa (African Development Bank), uliohusu kuanza kwa mradi uliowasilishwa na Baraza na kupitishwa na benki hiyo.
Mradi huo wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 15 unatarajiwa kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo ya pwani yaani Dar es Salaam, Pwani na Pemba.

Aidha, Dk Semesi alikutana pia na Sekretarieti ya Mfuko wa Kimataifa wa kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (Adaptation Fund-AF) ambapo aliweza kuwahimiza Adaptation Fund kukamilisha taratibu za kulipatia Baraza ithibati ya pili (reaccreditation) sambamba na kukamilisha mapitio ya miradi iliyowasilishwa yenye jumla ya thamani ya Dola za Marekani milioni 35.
Katika mazungumzo hayo, mfuko wa Adaptation Fund umelihakikishia Baraza kwamba taratibu za ithibati zitakamilika ndani ya wiki chache kuelekea mwishoni mwa mwaka huu.
Hata hivyo Adaptation Fund umeidhinisha ripoti za mwaka za miradi ya SWAHAT na Bunda inayosimamiwa na Baraza Pamoja na kuachilia kiasi cha takribani Dola za Marekani laki 4 ili kukamilisha utekelezaji wa miradi hiyo.

Sambamba na hayo, Dk Semesi ameongoza ushiriki katika vikao mbalimbali vya kitaalam, mikutano ya pembezoni pamoja na kuanzisha mchakato wa mashirikiano na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi ili kupanua wigo wa kujipatia fedha za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Baadhi ya taasisi hizo ni pamoja na Mfuko wa Kitaifa wa Maji (National Water Fund), Pew Charitable Trust, Benki ya Dunia, Global Climate Mobility, Global Methen Hub, IUCN na Ocean Vision.
Timu ya wataalam iliyoambatana na ujumbe wa Bodi kwenye Mkutano huo ni pamoja na Dk Careen Kahangwa, Fredrick Mulinda, Paul Kalokola, Jackline Nyantori na Rahim Kantinga.




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com