Tanzania, UNDCF kuendelea kushirikiana LoCAL II

SHIRIKA la Maendeleo ya Mfuko wa Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNDCF) limekubali kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza Programu ya LoCAL awamu ya pili.

Kupitia Programu hiyo Serikali inatekeleza miradi yenye thamani ya dola milioni 11 katika halmashauri 18 Tanzania Bara na Zanzibar.

Hayo yamejiri katika Mkutano wa Uwili kati ya Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Abdallah Hassan Mitawi na Afisa kutoka Shirika la UNCDF, Damiano Borgogno.

Mazungumzo hayo yamefanyika wakati wa Mkutano wa 30 wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP30) unaofanyika katika Jiji la Belem, Brazil.

Katika mazungumzo yao, pia UNCDF imeonyesha nia ya kushirikiana na Tanzania katika maeneo mengine yanahusiana na hifadhi ya mazingira.

Eneo mojawapo ni la Uchumi wa Buluu ambalo ni sekta muhimu inayokua kwa kasi na kuchochea uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla endapo rasilimali zake zitatumiwa ipasavyo.

Ofisi ya Makamu wa Rais tayari imeanzisha Kitengo maalumu cha kuratibu Uchumi wa Buluu na inaendelea kuratibu na kutekeleza Sera ya Uchumi wa Buluu (2024) na Mkakati wake.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button