Chongolo aahidi kutimiza malengo Wizara ya Kilimo

WAZIRI wa Kilimo, Daniel Chongolo ameieleza menejimenti na watumishi wa wizara hiyo kuwa kazi na malengo yaliyopangwa yatafi kiwa kwa kuendeleza pale mtangulizi wake, Hussein Bashe alipoishia ili kukuza na kuleta tija kwenye kilimo.
Chongolo alisema hayo wakati akizungumza kwenye makabidhiano ya ofisi na Bashe jijini Dodoma. Alimpongeza Bashe, menejimenti na watumishi wa wizara kwa kuwa mstari wa mbele kwa kubuni miradi ambayo imekuwa ikileta tija na manufaa kwa wakulima na taifa. SOMA: Wanawake wanavyochangamkia kilimo ikolojia kuzalisha mazao ya asili
Hafla hiyo imehudhuriwa pia Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde; Katibu Mkuu, Gerald Mweli na Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Umwagiliaji na Zana za Kilimo, Athumani Kilundumya pamoja na wakurugenzi wakuu wa taasisi za wizara ya kilimo zilizopo Dodoma.
Kupitia hafla hiyo, Bashe alimpongeza Chongolo kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo na kumhakikishia ushirikiano wakati wowote katika kufanikisha maono makubwa ya Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya kilimo.



