Karne moja baada ya kugawanywa Afrika
Vita vipya ni kwa ajili ya nguvu ya dunia

DAR ES SALAAM: Karne moja baada ya Ulaya kulitawanya Bara la Afrika katika kile kilichoitwa “Scramble for Africa,” ushindani mpya wa kijiografia unaibuka wakati huu ukiwa wa kimataifa, lakini mizizi yake ikiwa tena kwenye madini muhimu ya Afrika.
Kutoka mashamba ya ‘cobalt’ Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hadi korido mpya za ‘rare earth’ na ‘graphite’ nchini Tanzania, mataifa makubwa yanajipanga upya katika mbio ambazo wachambuzi wa Afrika wanaonya zinafanana kwa kiasi kikubwa na mbinu za kulazimisha za enzi ile ya mwanzo. Zana zimebadilika, diplomasia, ushirikiano wa usalama, na shinikizo la kifedha lakini nia, wanasema ile ile.
Madini ya cobalt, coltan ya Congo hayajawaletea wananchi utajiri wala manufaa yoyote makubwa, badala yake, rasilimali hizo zimegeuka kuwa uwanja wa vita ambapo makundi ya wanamgambo yakihusishwa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na maslahi ya nje.
Kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu DRC lilisema katika tathmini yake ya 2023 kwamba “minyororo ya ugavi wa madini bado inatoa mapato kwa makundi ya waasi na watu walio na uhusiano na wanasiasa na wafanyabiashara.”
Kiongozi mmoja wa asasi za kiraia wa Congo alieleza kwa uchungu: “Madini yetu ni baraka kwa kila mtu isipokuwa kwa wenye ardhi.”
Mfumo huu wa shinikizo la kimkakati hauishii tu kwenye maeneo yenye vita. Unajirudia katika nchi ambazo utulivu na uimara wa taasisi zao ulitarajiwa kuwa ngao.
Tanzania sasa imejikuta ikivutwa na wakati mwingine ikisukumwa na mataifa yanayotaka kupata fursa za muda mrefu. Ubalozi unaongezeka, ahadi za uwekezaji zinaongezeka, na ushirikiano wa kitaalamu unatanuka, lakini nyuma ya lugha ya “ushirikiano” kuna harakati zisizofichika
Hayati Kwame Nkrumah alionya mwaka 1965 kwamba “ukoloni mamboleo ni aina mbaya zaidi ya ubeberu kwa sababu unatoa picha ya uongo ya uhuru.”
Kauli yake inatoa mwangwi mpya wakati mataifa ya Magharibi, China na Mashariki ya Kati yakiongeza ushindani wa kupata madini muhimu kwa utengenezaji wa semiconductors, magari ya umeme na teknolojia za kijeshi za vizazi vijavyo. Afrika si mpakani tu pa rasilimali imekuwa uwanja muhimu wa mapambano ya kimataifa ya uzalishaji na uimara wa kisiasa.
Tanzania, inayoheshimika kwa uthabiti wake wa kisiasa, sasa inakabiliwa na mashinikizo ya kutaka irekebishe kanuni za udhibiti wa rasilimali na kutoa leseni za muda mrefu.
Katika miaka ya 1970, Julius Nyerere alionya dhidi ya misaada ya kigeni inayokuja kwa sura ya urafiki ilhali lengo lake ni ushawishi, akisema: “Tuwe waangalifu na shinikizo za kificho zinazokuja kwa jina la msaada au urafiki; nia huwa si ushirikiano, bali ni ushawishi.” Kauli hiyo inabaki kuwa halisi wakati mataifa ya nje yanapopinga sera zinazotanguliza uwezeshaji wa ndani, uongezaji thamani na udhibiti wa taifa.
Ushirikiano wa kiusalama unaongeza tabaka lingine. Marekani inadai kwamba AFRICOM ipo kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugaidi na usalama wa baharini pekee. Lakini wakosoaji kama Profesa Horace Campbell wanasema kwamba ongezeko la vituo vyake barani linaonekana zaidi katika maeneo yenye utajiri wa madini, wakionya juu ya “kijeshi wa sera ya Marekani barani Afrika kwa kivuli cha usalama huku maslahi ya kiuchumi yakifuatwa.” Washington inakanusha kuwa na maslahi ya rasilimali, lakini mtazamo huo tayari umejikita kutoka Dar es Salaam hadi Kinshasa.
Nyuma ya mahusiano ya kijeshi, kuna zana za kiuchumi zisizoonekana kirahisi. Mashirika ya utoaji tathmini za kiuchumi, taasisi za ufuatiliaji wa uzingatiaji, na wafadhili huathiri namna mitaji inavyoingia katika masoko ya Afrika. Serikali zinapojaribu kupanua ushirikiano na mataifa yasiyo ya Magharibi, mara moja huibuka onyo kuhusu “hatari ya madeni,” “mwelekeo wa kiimla,” au “mikataba isiyo wazi.”
Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limeonya mara kwa mara kuwa mataifa ya nje “yanaingilia michakato ya kisiasa ya ndani kwa jina la msaada,” jambo ambalo viongozi wengi wa Afrika wanasema linadhoofisha mamlaka ya bara.
Mfumo huu wa ushawishi hauji kwa sauti kubwa. Unakuja kupitia masharti ya mikopo, msaada wa kitaalamu, taratibu za NGOs, kanuni za usuluhishi wa uwekezaji, na shinikizo la kidiplomasia lililopambwa kwa lugha ya maendeleo. Mwanadiplomasia mmoja wa Afrika Mashariki alieleza kwa ukali: “Ukifuata wanachotaka, wanakuita mshirika; ukijadiliana, wanakuita tatizo.”
Kwa Waafrika wengi, mienendo hii inaakisi kile Frantz Fanon alichokiita “mashubaka yaliyosalia ya ubeberu ambayo lazima yatambuliwe na kuondolewa.” Leo, mashubaka hayo yanaonekana katika viashiria vya utawala bora, miungano ya kiusalama, na simulizi zinazowakilisha kujitegemea kwa Afrika kama ishara ya vurugu au kutokuwa thabiti. Mataifa ya Afrika yanapotaka mikataba isiyo na upendeleo au kuongeza thamani nchini, wakosoaji huita hatua hizo “utaifa wa rasilimali”ingawa haya ni mambo yanayotekelezwa kikawaida katika nchi zilizoendelea.
Hata hivyo, bara haliko tulivu. Tanzania, Namibia, Zambia, Botswana, Rwanda na Afrika Kusini zinaimarisha sheria za madini, zinapitia upya mikataba ya zamani, na kusisitiza usindikaji ndani ya nchi. Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA), ingawa bado kwenye hatua ya utekelezaji, linatoa njia ya kuepuka majadiliano yaliyogawanyika yaliyoliangamiza bara katika zama za awali za rasilimali. Harakati za vijana, fikra za kisera, na asasi za kiraia zinaibuka kwa nguvu zikidai Afrika iwe mwamuzi wa bei, si mpokeaji tu.
Nyerere aliukumbusha ulimwengu: “Afrika haitaki mabaki kutoka mezani mwa tajiri; sisi ndio wazalishaji wa utajiri wa dunia, ni lazima tuudhibiti.” Kauli yake inaeleza uzito wa wakati huu. Mabadiliko ya dunia kuelekea nishati safi, miundombinu ya kidijitali, na uzalishaji wa teknolojia ya hali ya juu hayawezekani bila madini ya Afrika. Lakini bila utawala imara na mkakati wa pamoja, Afrika inaweza kurudia historia ile ile chungu.
Scramble mpya ya Afrika imewasili lakini pia Afrika mpya imezaliwa: yenye uelewa zaidi, yenye uthubutu na isiyotaka tena kuendeshwa. Karne moja baada ya kugawanywa kwa bara, vita havihusiani tena na Afrika pekee. Ni mapambano ya nguvu za dunia na mara nyingine tena, Afrika iko katikati yake.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com