Mafuriko yauwa watu 81

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Kenya (KMD) imesema mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi imesababisha mafuriko makubwa na kusababisha vifo vya watu 81 ndani ya mwezi huu.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, mvua hizo zinaendelea kunyesha katika sehemu nyingi nchini humo huku kanda ya Magharibi ikiathirika zaidi. Taarifa zinasema kuwa baadhi ya maeneo ya vijiji katika Kaunti ya Kisumu vimezamishwa na maji huku zaidi ya hekari 1,200 za mashamba zikiharibiwa na  kusombwa na mafuriko.

Mpaka sasa zaidi ya familia 3,000 zimelazimika kuhama makazi yao katika eneo la Nyakach ambapo baadhi yao wamepata hifadhi katika vituo nane vilivyoandaliwa kusaidia waathirika. Hatahivyo, maji yanayomwagika kutoka Mto Mirui yanaendelea kutishia usalama wa raia katika maeneo hayo.

Hadi sasa mji mkuu wa Nairobi ndio ulioripoti idadi kubwa ya vifo ambapo watu 37 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko. SOMA: ‘Tumieni taarifa sahihi za hali ya hewa’

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button