Marburg yaua sita Ethiopia

IDADI ya vifo vinavyotokana na mlipuko wa virusi vya Marburg nchini Ethiopia imeongezeka na kufikia watu sita, kwa mujibu wa taarifa iliyothibitishwa na Shirika la Habari la Ethiopia.
Ethiopia imeripoti mlipuko huo kwa mara ya kwanza Novemba 14, ikiwa ni tukio la kwanza la ugonjwa wa Marburg kutokea nchini humo. Tangu kutangazwa kwa mlipuko, jumla ya watu 11 wamethibitika kuambukizwa virusi hivyo, huku baadhi yao wakiendelea kupokea matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na Shirika la Habari la Reuters, Wizara ya Afya ya Ethiopia imewatenga watu 349 waliodhaniwa kuwa na mawasiliano ya karibu na wagonjwa, na kati yao 119 tayari wameruhusiwa baada ya kukamilisha kipindi cha uchunguzi.
Virusi vya Marburg, ambavyo vinatoka katika familia moja na Ebola, husababisha homa kali, maumivu makali ya kichwa, na katika baadhi ya matukio kusababisha kutokwa na damu ndani na nje ya mwili. SOMA: Ebola yaibuka tena Congo



