Ujenzi madaraja barabara ya Kusini wafika patamu

WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amekagua na kuridhishwa na hatua mbalimbali za ujenzi wa madaraja ya dharura yaliyoko katika Mkoa wa Lindi ambayo utekelezaji wake umefikia zaidi ya asilimia 88.

Baadhi ya madaraja hayo ni yale yaliyojengwa katika maeneo ya Somanga, Njia Nne na Matandu ambako kuharibika kwa barabara katika maeneo hayo wakati wa majira ya mvua kulikuwa kunasababisha usafiri wa kwenda mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma mgumu.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Ulega aliwahakikishia Watanzania kuwa madaraja hayo yatakapokuwa yamekamilika kwa asilimia 100, mambo yaliyokuwa yakitokea miaka yote kipindi cha mvua za masika katika eneo la Somanga, Njia Nne na Matandu hayatarejea tena.

SOMA: Ulega ataka kasi ujenzi miundombinu Dodoma

Katika hatua nyingine, Ulega amewahakikisha Watanzania kuwa wakandarasi hawatalala bali watafanya kazi usiku na mchana ili hadi kufikia Disemba 24, 2025 madaraja hayo yawe yamekamilika.

Waziri Ulega amekagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Somanga Mtama (m 60) ambalo limefikia asilimia 89, Daraja la Kipatwa (m 40) limefikia asilimia 86.7, Daraja la Mikereng’ende (m 40) limefikia asilimia 90.06 na Daraja la Njenga (Matandu) lenye urefu wa mita 60 ambalo limefikia asilimia 86.67.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mohammed Nyundo, ametoa pongezi kwa Waziri Ulega pamoja na timu ya wataalamu kutoka wizarani na TANROADS kwa ujenzi wa madaraja hayo ambayo hivi sasa kazi kubwa zote zimekamilika. Pia alisema wameambiwa kuwa wananchi wataruhusiwa kupita kwenye madaraja hayo pale mvua zitakapokuwa zimeanza.

Naye, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi, Emil Zengo, amefafanua kuwa katika Daraja la Somanga Mtama (m 60), mkandarasi amekamilisha ujenzi wa nguzo 43 zenye urefu wa mita 12, nguzo kuu tatu zinazobeba daraja, boriti za chuma na ameshamaliza kusuka nondo katika kitako cha daraja kwa ajili ya kumwaga zege.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button