Posta Tanzania yatunukiwa cheti usalama UPU

SHIRIKA la Posta Tanzania limetunukiwa Cheti cha Usalama cha Kimataifa (S58 & S59) kutoka Umoja wa Posta Duniani (UPU), kufuatia mafanikio katika zoezi la tathmini ya usalama wa mifumo, miundombinu na taratibu za utoaji huduma lililokamilika Novemba 7, 2025.

Cheti hicho cha Daraja “A” tuzo ya dhahabu kimetolewa rasmi Novemba 24, 2025, na Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Posta Duniani UPU, Masahiko Metoki, mara baada ya timu ya wataalamu wa UPU kufanya ukaguzi wa kina wa wiki moja uliolenga kuhakiki viwango vya usalama wa Shirika katika kulinda mizigo, barua na taarifa nyeti zinazopitia katika mnyororo wa huduma za posta.

Katika zoezi hilo la tathmini, Shirika la Posta Tanzania limepata alama 598 kati ya 640, likitimiza kwa ufanisi vigezo vyote vya kupewa cheti hicho cha heshima kinachotolewa kwa taasisi za posta zinazofikia viwango vya juu vya usalama wa kimataifa.

Wakipokea cheti hicho, Caroline Kanuti kwa niaba ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mambo ya Ndani ya Shirika, S.P. Mathias Kipeta, wameishukuru UPU kwa kutambua juhudi kubwa zinazofanywa na Shirika katika kuimarisha usalama wa huduma zake, na kuahidi kuendeleza maboresho endelevu katika mifumo na miundombinu ya Shirika.

Aidha, wataalamu wa UPU waliwasilisha mapendekezo ya kuongeza ufanisi zaidi katika maeneo ya udhibiti wa mizigo, ufuatiliaji wa usafirishaji wa barua na vifurushi, pamoja na uboreshaji wa vituo vya kuchakata mizigo (Office of Exchange) ili kuhakikisha huduma bora, salama na za kisasa.

Kupitia mafanikio haya, Posta Tanzania sasa imeorodheshwa rasmi miongoni mwa waendeshaji wa huduma za posta duniani waliotunukiwa cheti cha usalama na UPU hatua inayoliweka Shirika katika nafasi ya juu kimataifa na kuimarisha uaminifu, ushindani na ubora wa huduma kwa wananchi na wateja wa kimataifa.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button