Sendiga ataka uwajibikaji Manyara

MANYARA: Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amewaagiza watendaji wa kata katika kata zote 142 zilizopo mkoani Manyara kuandaa taarifa sahihi za kata ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuongeza uwajibikaji.
Akizungumza na waandishi wa habari, Sendiga amesema ni muhimu watendaji wa kata husika kuwa na taarifa sahihi za maendeleo na miradi wanayoisimamia kwa kuwa itakaguliwa na kuchukua hatua kwa miradi kichefuchefu.
Ziara ya kikazi imeanza leo Disemba 4, 2025 kutembelea kata zilizopo Wilaya ya Hanang na kuhusisha wataalamu wa sekta mbalimbali kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kujenga uelewa,uwazi na uwajibikaji
”Tutakwenda kata kwa kata kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kufanya mikutano ya hadhara kwenye kata husika,”amesema Sendiga.
Amesema msimu huu wa pili wa kampeni ya ‘Tunavua buti hatuvui tukutane site’ni ya kuangalia utekelezaji wa Kauli mbiu hii inayotupa sisi watumishi kuhimiza uwajibikaji na kuweka mikakati ya kutatua changamoto, ukaguzi wa miradi ya maji,elimu,afya, ujenzi pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Kwa mujibu wa Sendiga imekuwa ni mazoea ya wananchi kukimbilia ofisi ya mkuu wa mkoa kuleta kero zao ili zitatuliwe wakati kuna ngazi ya watendaji wa kata imerukwa jambo ambalo amesema si sahihi.




I am making a good salary from home $7580-$9065/week , which is amazing, under a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions, Definitely a try..
See This Link………………………………….. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com