Visiwa Ziwa Victoria vitakavyofaidi ushirikiano nishati safi

“HUU ni ukombozi dhidi ya madhara kwa wanawake na watu wengine yanayotokana na moshi utokanao na matumizi ya muda mrefu ya kuni, sambamba na watu hao kutumia muda mwingi na gharama kubwa za fedha kutafuta kuni na mkaa, badala ya kufanya shughuli za uzalishaji mali.
“Mpango huu utaboresha huduma za afya katika zahanati na maduka ya dawa, maabara ndogondogo kwa kutoa mwanga wakati wa kutoa huduma za afya, zikiwamo za wajawazito kujifungua pamoja na kuhifadhi dawa na chanjo.” Hayo yanasemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kitanzania ya PowerHut Renewables Limited, Dk Prosper Magali akifafanua taarifa kuhusu kampuni hiyo ya mjini Arusha kuingia mkataba wa mwaka mmoja wa ushirikano wa kimkakati baina yake na Shirika la Assist International na kampuni ya Caterpillar Inc; zote za Marekani pamoja na Mantrac ya Tanzania.
Ushirikiano huo unalenga kuunga mkono upatikanaji wa umeme wa uhakika, gharama nafuu, endelevu, jumuishi na nishati safi ya kupikia kwa kuongeza upatikanaji wa huduma za umeme katika visiwa vinne vya Kasalazi, Juma, Ziragula na Bezi vilivyopo katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa Dk Magali, miongoni mwa walengwa na wanufaika wakuu wa mradi huo ni wajasiriamali, wakiwamo wa ufundi wa fani mbalimbali kama useremala na uchomeleaji vyuma.
“Moja ya maboresho hayo ni kuwezesha miundombinu hiyo ya nishati ya umeme kuchaji betri zinazotumiwa na wavuvi kuvua samaki na kuwezesha uhifadhi wa mazao ya samaki, kwa kutumia miundombinu inayotumia umeme kama majokofu pamoja na kugandisha barafu kwa ajili ya kazi hiyo,” anasema Dk Magali.
Anaongeza: “Unajua, mkakati huu unalenga hasa kuunga mkono juhudi za serikali kuchochea matumizi ya nishati safi ya kupikia, kulinda afya za watu na kukabili uharibifu wa mazingira kwa kuwezesha wakazi wa visiwa hivyo kupata kirahisi na kutumia nishati safi ya kupikia na kufanyia shughuli nyingine, zikiwamo za ujasiriamali.”
“Ikumbukwe visiwani kuna changamoto kubwa ya kupata kuni na mkaa, maana visiwa vingi havina kuni wala mkaa badala yake, wanategemea kununua kutoka nchi kavu,” anasema.
Kwa mujibu wa Dk Magali, ushirikiano huo utaboresha miundombinu ya uzalishaji na usambazaji wa umeme katika visiwa hivyo ili kumudu mahitaji ya nishati hiyo yanayoendelea kuongezeka visiwani humo, hasa katika uzalishaji mali kwa kutumia umeme.
“Matamanio ya watu ya kuboreshwa kwa huduma za umeme sasa yanashughulikiwa,” anasema.

Katika taarifa yao ya pamoja, Makamu wa Rais wa Program na Mikakati wa Assist International, Cheri Reynolds anasema: “Umeme wa uhakika hujenga uwezekano mpya katika familia na jamii; huwezesha watoto kusoma hata giza linapoingia, vituo vya huduma za afya vinaweza kuhudumia wagonjwa kwa uhakika na biashara ndogo zinaweza kupanuka na kukua.”
Anaongeza: “Assist International imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania kwa miaka mingi na kushuhudia nguvu ya ubia katika kuleta mabadiliko chanya na endelevu… Tumevutiwa kujiunga katika ushirikiano huu kuleta nishati inayojitegemea kusaidia elimu, huduma za afya na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.
Reynolds anasema yote hayo yanafanyika kupitia mpango wa huduma za umeme wa Kampuni ya Caterpillar Inc.
Huo ni mpango wa uhisani unaolenga kupeleka huduma za umeme katika maeneo mbalimbali ya Afrika, kwa kutumia teknolojia madhubuti za Caterpillar ukisimamiwa na Assist International ambalo ni shirika lisilo la kiserikali la Marekani, linalosambaza shughuli za kimkakati na endelevu duniani kote zikiwemo huduma za nishati.
Makamu wa Rais wa Caterpillar Inc. katika Kitengo cha Umeme, Mellissa Busen anasema: “Kupata umeme wa uhakika nchini Tanzania ni zaidi ya miundombinu, ni hasa kuwezesha jamii, kuimarisha usalama na kufungua fursa.”
Anaongeza: “Ushirikiano huu unaakisi kujitoa kwa Caterpillar na Mantrac kwa ajili ya Watanzania na kuhakikisha tunachangia kujenga ulimwengu endelevu zaidi.”
Naye Meneja Usimamizi wa Biashara kwa Afrika Mashariki wa Mantrac Tanzania, Amr Zaki anasema, “Tunaona fahari kuunganisha nguvu na kampuni za PowerHut, Caterpillar na Assist International kuleta suluhisho endelevu la nishati ili kusaidia mabadiliko ya maisha na kuimarisha uhimilivu wa ndani.”
Anaongeza: “Katika utekelezaji wa ushirikiano huo wa mwaka mmoja tangu Desemba 4, 2025… Kampuni ya PowerHut Renewables Limited ndiyo inayomiliki na kushughulikia miundombinu na shughuli za kila siku za uzalishaji umeme na uendeshaji katika visiwa hivyo.”
Anaendelea, “Wadau wengine (kampuni hizo) kwa pamoja watatoa fedha na teknolojia katika kufanya uboreshaji unaokusudiwa.
“Tunatarajia kupata ushirikiano mkubwa kutoka serikalini, wizara husika na taasisi zake na wadau wengine ili kuhakikisha mpango huu unatekelezwa kwa mafanikio na kunufaisha wananchi katika visiwa hivyo”.
Imebainika pia kuwa, Kampuni ya PowerHut Renewables Limited ina miradi minane ya kuzalisha na kusambaza umeme katika visiwa kwa kutumia umemejua na kuusambaza kwa kutumia gridi ndogo tangu mwaka 2018.
Mkurugenzi mtendaji wa PowerHut Renewables Limited anabainisha kuwa, miradi hiyo inatoa huduma za umeme kwa wakazi zaidi ya 2,000 katika visiwa vya Juma, Kasalazi, Ziragula, Bezi, Yozu, Chembaya, Sozia na Lyegoba katika Ziwa Victoria.
“Tulibaini kuwa, mahitaji ya umeme yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka na hivyo, kulazimika kutafuta na hatimaye kupata wadau wa kufanya uboreshaji unaokusudiwa ili kukidhi mahitaji ya watu,” anasema Dk Magali.




https://www.bbc.com/swahili/medianuai/2012/11/121110_kisa_mkasa101112
Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
.
Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com
UTEUZI
https://www.bbc.com/swahili/medianuai/2012/11/121110_kisa_mkasa101112
Industrialization £56,565,656,000 available
https://www.bbc.com/swahili/medianuai/2012/11/121110_kisa_mkasa101112
Industrialization £56,565,656,000 available for job creation
https://www.bbc.com/swahili/medianuai/2012/11/121110_kisa_mkasa101112