ACT kujadili uchaguzi mitaa

CHAMA cha ACT-Wazalendo kinatarajiwa kufanya kikao cha Halmashauri Kuu kitachojikita katika kujipanga kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu Mwenezi wa chama hicho, Shangwe Ayo kikao hicho kitafanyika Agosti 25, kitatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu kitachokutana Agosti 24, vikao vyote vitafanyika makao makuu ya chama hicho Magomeni, Dar es salaam.

Shangwe amesema mbali na Agenda ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vikao hivyo vitapokea taarifa ya utekelezaji wa programu za chama katika kipindi cha miezi sita iliyopita na kupanga programu za chama katika kipindi cha miezi sita ijayo.

“Pia kikao hicho kitapokea taarifa juu ya utekelezaji wa Azimio la Halmashauri Kuu iliyopita la kujitoa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar,” imeeleza taarifa hiyo.

Kikao cha Halmashauri Kuu kinatarajiwa pia kujaza nafasi za manaibu katibu wakuu Bara na Zanzibar ambao hawakuteuliwa kwenye kikao kilichopita.

SOMA: ACT Wazalendo waivuruga Chadema Lindi

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

Habari Zifananazo

Back to top button