ACT Wazalendo yavuna CCM, CUF Mchinga
Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4720
LINDI; BAADHI ya wanachama wa Chama Cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Mchinga Wilaya ya Lindi Mjini mkoani Lindi wamejiunga na Chama Cha ACT Wazalendo, Makamu Mwenyekiti Bara, Isihaka Mchinjita amethibitisha.
Kwa mujibu wa Mchinjita, wanachama hao wameamua kujiunga na ACT Wazalendo, wakiamini kuwa chama hicho kitawakilisha maslahi yao kwa uadilifu na uwazi.
Akizungumza na HabariLEO kutoka mkoani humo, Mchinjita amesema wanachama hao wamesema wamechoshwa na ulaghai wa kisiasa.
Soma pia: Vigogo ACT Wazalendo kuzunguka majimbo 125
Amesema baada ya wanachama hao kujiunga na chama hicho, walimuomba mwenyekiti huyo kufanya ziara maalum jimbo zima la Mchinga ili kuwapokea rasmi wanachama wapya na kujadiliana nao kuhusu mikakati ya maendeleo ya kisiasa na kiuchumi katika eneo hilo.
“Ziara hii inatarajiwa kuleta ari mpya na ushirikiano imara miongoni mwa wanachama wa ACT Wazalendo jimboni humo,” amesema Mchinjita.
Deprecated: htmlspecialchars(): Passing null to parameter #1 ($string) of type string is deprecated in /home/habarileoacc/public_html/wp-includes/formatting.php on line 4720