CCM kutoa msukumo mradi wa maji Bunda

BUNDA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitahakikisha kinatoa msukumo kwa serikali ili kuhakikisha mradi mradi wa maji kutoka Butiama hadi Nyamuswa unakamilika kwa wakati ili kutimiza azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya Kumtua mama ndoo kichwani.
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Magunzo wa CCM, Kihongosi ameeleza hayo leo Mei 17,2026 alipokagua mradi wa Butiama – Nyamswa katika Wilaya ya Bunda unaogharimu kiasi cha Sh bilioni nane katika utekelezaji wake, ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake mkoani Mara.

Akizungumza baada ya kujagua mradi huo Kihongosi amesema ni kazi kubwa imefanyika ya kutoa maji kutoka Butiama mpaka Nyamuswa na zaidi ya kilometa 21 au katika ulazaji wa mabomba na pampu ya eneo la nyamusa itasaidia kusukuma maji kupeleka kwenye tangi hilo na yaende kwa wananchi.
Amesema hatua hiyo tayari ni dhamira njema ya serikali akiwaahidi wananchi wa eneo hilo kuwa kwa chama kimeshiriki katika utekelezaji wataipa msukumo Wizara ya Maji ili kuhakikisha jambo hilo halishindikani kwakuwa dhamira ya Rais ni kumtua mama ndoo kichwani.

“Tutaongea na Waziri Komredi Aweso tunajua anafanya kazi nzuri, jambo hili haliwezi likamshinda na kwa kuwa dhamira ya Mheshimiwa Rais ni kumtua mama ndoo kichwani ya maji naamini mradi huu utakamilika kwa mujibu wa mkataba kama ambavyo umeelekeza hapa,” amesema.
Awali, akisoma taarifa ya mradi huo Meneja Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)Wilaya ya Bunda, Esther Gilioma amesema utekelezaji wa mradi ni Sh bilioni 8.35, fedha zinazotolewa na Serikali tayari Sh bilioni mbili zimetolewa kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa mradi huo.

Mradi huo unahusisha uchimbaji na ulazaji wa mabomba yenye urefu wa mita 33,000, ujenzi wa matanki mawili ya maji yenye uwezo wa lita 300,000 na 200,000, pamoja na ujenzi wa ofisi za RUWASA na BUWSSA.
“Ujenzi wa tangi la maji la lita 200,000 umefikia asilimia 80 huku tangi kubwa la lita 300,000 pamoja na ofisi ya BUWSSA vikifikia asilimia tano ya utekelezaji. Kwa ujumla, mradi huu umefikia asilimia 60 na unatarajiwa kukamilika Juni 30, 2026 endapo fedha zitapatikana kwa wakati,” ameeleza Esther.



