Kihongosi ahamasisha wananchi kujiunga mifumo ya bima

ARUSHA: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa, Kenani Kihongosi amewahimiza wananchi kujiunga na mifumo ya bima ya afya ili kupunguza gharama za matibabu, huku akiwataka kupuuza propaganda zinazoweza kuwakatisha tamaa kuhusu umuhimu wa bima hiyo.

Kihongosi ameeleza hayo leo Juni 6,2026 alipotembelea na kushidiki kikao katika Shina Namba Mbili, Tawi la Naurei, Kata ya Sekei jijini Arusha mkoani Arusha, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini.

Kihohongosi ameeleza hayo akijibu ombi la wanachama wa shina hilo kuhusu msaada wa bima kwa wazee ili kusaidia kupata nafuu ya gharama za matibabu

Akizungumza hayo Kihongosi amesema kuhusu ombi la bima kwa wazee amesema hilo ni jambo la kisera na tayari serikali imeanza utekelezaji wake kwa baadhi ya mikoa, hivyo aliwataka wajitokeze kujiunga fursa hiyo itapowafikia.

“Hili ni jambo la kisera na serikali imeainisha na itaanza bima kwa watu wote na mpango huu utaanza mara moja na baada ya mikoa wameishaanza, kwa hiyo utakapoletwa kwetu, wachane na propaganda za wanasiasa, tendeeni tukajiunge kwenye mfumo wa bima,” amesema Kihongosi.

Ameongeza hiyo itasaidia kupunguza gharama za matibabu yetu kwa sababu mwingine anakuambia unachangia kiasi fulani hiyo hela serikali inachukua lakini ni bora uchangie kuliko gharama ikiwa kubwa peke yako hutaweza.

Awali akisoma ajenda za kikao hicho Katibu wa Shina Namba Mbili, Elinipa John amesema moja ya maombi ya shina hilo ni kuhusu upatikanaji wa bima za afya kwa wazee ili kuwasaidia kupata gharama za matibabu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button