Kihongosi asifu uongozi wa Dk Samia

ARUSHA: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Kihongosi, amesema uongozi wa taifa unahitaji uzoefu, utulivu na uwezo wa kufanya maamuzi makubwa, akisisitiza kuwa Tanzania inaendelea kunufaika na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amejijengea uzoefu wa muda mrefu katika utumishi wa umma.

Kihongosi amezungumza hayo leo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara leo Juni 5,2026 uliofanyika katika uwanja wa Kanisani Ngaramtoni wilayani Arumeru mkoani Arusha, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini.

Kihongosi amesema kuiongoza Tanzania kunahitaji kiongozi mwenye uwezo wa kusimamia masuala makubwa ya kitaifa na kuwaleta wananchi pamoja katika safari ya maendeleo na kiongozi huyo ni Rais samia Suluhu Hassan.

“Gari kubwa linahitaji dereva mzoefu, na dereva huyo ni Dk Samia Suluhu Hassan,” amesema Kihongosi.

Amesema tofauti na baadhi ya wanasiasa wanaotumia muda mwingi kujibu mashambulizi ya kisiasa kwa lugha zisizofaa na za matusi, Rais Samia ameendelea kuelekeza nguvu zake katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.

Kihongosi ameeleza kuwa uzoefu wa Rais Samia katika nyadhifa mbalimbali za uongozi umempa uwezo wa kuongoza nchi kwa utulivu huku akisimamia agenda za maendeleo katika sekta mbalimbali.

Aidha, amewataka wananchi kuendelea kuwaunga mkono viongozi wanaoweka mbele maslahi ya taifa na maendeleo ya wananchi badala ya siasa za hovyo, akisisitiza kuwa Tanzania inahitaji uongozi unaozingatia kazi, uwajibikaji na mshikamano wa kitaifa.

Amesema mafanikio yanayoendelea kushuhudiwa nchini ni ishara ya uongozi wenye dira na uzoefu, akiongeza kuwa CCM itaendelea kusimamia sera zake kwa lengo la kuimarisha maendeleo na ustawi wa Watanzania.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button