Adakwa kwa kuibia simu wagonjwa Mloganzila

DAR ES SALAAM; HOSPITALI ya Taifa Muhimbili, Tawi la Mloganzila imemkamata mtu mmoja kwa tuhuma za wizi wa mali, zikiwemo simu za mkononi tatu za wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.

Anayetuhumiwa ni Steven Julius ambaye amekuwa akijifanya mmoja ya waajiriwa katika hospitali hiyo kama Ofisa Muuguzi.

Julius amefikishwa katika Kituo cha Polisi Gogoni kilichopo Kibamba mkoani Dar es Salaam huku taratibu za kisheria zikiendelea.

Mtuhumiwa huyo alikiri mwenyewe kuhusuka katika wizi huo kwa kuiba simu tatu ambazo mbili aliziuza kwa mkazi wa Kibamba na nyingine ameiuza kwa mtu anayeishi nje ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Julius, baada ya kumaliza mafunzo kwa vitendo ya uuguzi aliwahi kufanya kazi katika hospitali kadhaa ambapo alifukuzwa kutokana na vitendo vya kukiuka maadili, ikiwemo wizi.

 

Habari Zifananazo

Back to top button