Trending

Afariki dunia muda mchache baada ya kuhesabiwa

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 60 mkazi wa kata  ya Majengo manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga amefariki dunia  saa chache baada ya kuhesabiwa na makarani wa sensa nyakati za usiku katika hospitali ya manispaa ya Kahama.

Pia mtu mwingine aliyekuwa amelazwa wodini katika hospitali hiyo  alikataa kuhesabiwa mpaka awaone viongozi wa eneo lake.

Akiongea na HabariLEO, Karani wa Sensa aliyefanya zoezi hilo  hospitalini  hapo  Robert Mayunga amesema kuwa zoezi limeenda  vizuri kwani walianza majira ya saa sita usiku kwa kuanzia hospitalini hapo.

Mayunga amesema kuwa mgonjwa aliyekuwa akikataa kuhesabiwa tayari ameshahesabiwa baada ya kupata maelezo na kujiridhisha na zoezi zima. Vilevile amesema, Mzee aliyefariki alikuwa na kijana wake  aliyetambulishwa kwa jina la Williams Shija ambaye pia alitoa maelezo  kabla mzee hajafariki dunia.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button