Afrika rejesheni amani Sudan
SUDAN : KAMISHNA Mkuu wa Shirika la umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi – UNHCR , Filippo Grandi amehoji mchakato wa urejeshwaji wa amani nchini Sudan ambapo kwa sasa vita vya wenyewe kwa wenyewe bado vinaendelea.
Grandi amesema tangu kuanza kwa vita mwezi Aprili mwaka 2023, zaidi ya watu milioni 10 wa Sudan wamelazimishwa kuyahama makazi yao, wakiwemo milioni mbili waliondoka nchini humo.
“Ni jambo la kutisha kusema kwamba kumekuwa na dhana, ambayo nadhani kwa bahati mbaya ni kweli, kuwa Afrika ina migogoro kila wakati. Sasa kumekuwa na aina ya mazoea, kuyachoka au kuyapuuza majanga hayo,”Grandi alisema.
SOMA : Sudan yakataa ujumbe wa umoja wa mataifa
Amesema hali ya Sudan kwa sasa inatia wasiwasi pale watu wanapoanza kukimbilia mataifa yasio jirani akielezea ongezeko kubwa la Wasudan takriban 40,000 wanaowasili nchini Uganda na wengine karibu 100,000 wakiwasili nchini Libya.