Ahadi za kampeni ziwe za kutekelezeka

KIJIWENI leo tupo na wananchi wa Mkoa wa Morogoro wakizunguza kuhusu kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025 zilizoanza tangu Agosti 29, 2025 mkoani humo.
Wananchi hao wamesema ni muhimu kwa mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan kutekeleza ahadi zake alizozitoa wakati alipozungumza na wananchi hao. Enock Peter anasema serikali imetoa ahadi kuboresha miundombinu ya maji na barabara, hivyo wanaiomba serikali kutekeleza ahadi hizo. SOMA: Fadhili Ngajilo ajitosa ubunge Iringa Mjini ataja ahadi 10 mageuzi
Alisema kama ahadi hazitafanyiwa kazi wananchi wataona kama ahadi wanazopewa ni ‘siasa’ tu. Mkazi wa Ulanga, Hassan Seleman amesema shida kubwa katika eneo lake ni ubovu wa barabara. “Barabara ni kilio kikubwa sana kwa wananchi, tunaomba serikali kufanya ukarabati wa barabara.



