Ahmadiyya yawafariji wenye uhitaji Moro

MOROGORO: JUMUIYA ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania imetoa vyakula katikakaya zaidi ya 200 zenye uhitaji zinazoishi Kata ya Kihonda Maghorofani Manispaa ya Morogoro ikiwa ni zawadi ya mkono wa Eid El- Fitri.
Naibu Amiri wa Jumuiya hiyo nchini , Sheikh Abid Mahmood Bhatti , amesema hayo wakati wa kugawa vyakula hivyo ambayo ni mchele na unga wa sembe kwa kaya kaya zenye uhitaji kutoka mitaa tisa ya kata hiyo.

Sheikh Bhatti amesema kaya zilizopatiwa vyakula hivyo ni kutoka mitaa ya Ngerengere, Kitata, Msamvu B, Airport ,Kihonda Maghorofani “A” na “B” , Godes , Bima na Mbuyuni jambo ambalo hufanyika kila mwaka.
Bhatti ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Cha Jamia Ahmadiyya Tanzania amesema zawadi ulioyolewa ni unga kilo tano na mchele kilo tano kwa kaya na ni utaratibu unaofanyika kila mwaka.
“Kidogo ulichonacho unakitoa kwa muhitaji na kikampatia tabasamu, kile kitendo cha muhitaji kutabasamu ni baraka kwa Mungu haijalishi hata kama utampatia Sh 500 tu au kilo moja ya unga”amesema Sheikh Bhatti.
Naibu Amiri wa Jumuiya hiyo nchini ametoa rai kwa taasisi na watu binafsi ambao wanauwezo kujitokeza kusaidia kaya zenye uhitaji hasa kipindi hiki cha sikukuu ili kuwa fanya kusherehekea sawa na walichonacho.

“Watu ni familia ya mwenyezi Mungu, na mpendwa wa mwenyezi Mungu ni yule ambaye anainufaisha familia ya mwenyezi Mungu pia Mtume wetu anatufundisha kwamba mwenyezi Mungu anaendelea kumsaidia mtu yule ambaye anawasaidia watu wake,” amesema Sheikh Bhatti.
Naibu Amiri wa Jumuiya hiyo amesema kuwa lengo ni kuunga mkono wito wa Serikali inayohimiza mashirika, taasisi,na watu binafsi kutoa misaada kwa jamii yenye uhitaji.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Khalid Matengo ameishukuru jumuiya hiyo kwa kutoa msaada wa vyakula kwa wananchi hivyo viongozi wake wameonesha utu na kuongeza ushirikiano na jamii inayowazunguka.

Matengo amesema mbali na zawadi hiyo pia Jumuiya hiyo imekuwa mshirika mzuri wa maendeleo katika jamii hasa katika kuchangia shughuli za maendeleo ikiwemo miundombinu ya barabara za kata hiyo na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule zilizoribu na chuo hicho.
Baadhi ya walengwa akiwemo Mwanahamisi Madebe ambaye mkazi wa mtaa wa Msamvu B ameishukuru Jumuiya hiyo kwa kuwapatia msaada huo na kupunguza gharama za mahitaji ya chakula hasa wakati wa sikukuu.



JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com