Ahmed Al-Sharaa ateuliwa Rais wa mpito Syria

SYRIA: ALIYEKUWA kiongozi wa kundi la Hayat Tahrir al-Sham (HTS), Ahmed Al-Sharaa, ameteuliwa kuwa Rais wa mpito wa Syria, kufuatia kuondolewa kwa Bashar al-Assad kutoka madarakani.

Mamlaka mpya ya Syria imetangaza kuwa Al-Sharaa atachukua uongozi wa nchi hiyo baada ya kiongozi wa muda mrefu Bashar al-Assad kuondolewa.

Muungano wa waasi unaoongozwa na Al-Sharaa wa kundi la Hayat Tahrir al-Sham ulifanya mashambulizi makali na kumtimua Assad mnamo Desemba 8, kumaliza utawala wa miongo mitano wa familia ya Assad.

Baada ya kuanguka kwa serikali ya Assad, waasi walitangaza serikali ya mpito chini ya Mohammad al-Bashir ambayo itaongoza hadi Machi 1.

Shirika la habari la serikali ya Syria limeripoti kuwa Al-Sharaa amepewa jukumu la kuunda baraza la kutunga sheria hadi katiba ya kudumu itakapopitishwa.

Bunge la Assad limevunjwa na katiba ya 2012 imejumuishwa, huku makundi yote ya kijeshi yakivunjwa na kuunganishwa katika taasisi za serikali. SOMA: Uchaguzi huru ufanyike Syria- UN

Aidha, jeshi la Assad na mashirika ya usalama yamevunjwa, na chama cha Baath kilichokuwa kikitawala Syria kwa miongo kadhaa kimeondolewa.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button