SYRIA : MJUMBE maalum wa Umoja wa Mataifa Geir Pedersen ametoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki nchini Syria.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Damascus, Pedersen amesema kuna matumaini makubwa juu ya Syria mpya, ambayo ameeleza itajumuisha suluhisho la kisiasa katika eneo linaloshikiliwa na wakurdi kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.
Pia amesisitiza umuhimu wa kupelekwa misaada ya kibinadamu nchini humo baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais Bashar al-Assad. SOMA: Mchakato wa kisiasa jumuishi uanzishwe
Hatahivyo, amehimiza kuundwa kwa Syria mpya, sambamba na azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa nambari 2254, na kwamba kutafanyika uchaguzi huru baada ya kipindi cha mpito.
Azimio nambari 2254 lililopitishwa mwaka 2015 wakati wa kilele cha vita vya wenyewe kwa wenyewe, lilitoa njia ya kuelekea kupatikana kwa suluhisho la kisiasa nchini Syria.