Airtel Afrika yajivunia ufanisi robo ya kwanza 2025

Dar es Salaam: Airtel Africa imetangaza matokeo bora kwa robo ya kwanza iliyoishia Juni 30, 2025, ikionesha ongezeko la wateja wanaotumia huduma za intaneti na Airtel Money katika nchi mbalimbali za Afrika.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Airtel Africa, Sunil Taldar, amesisitiza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya utekelezaji wa mkakati thabiti unaolenga kuboresha huduma kwa wateja na kuwekeza katika teknolojia mpya kama vile Airtel Spam Alert ili kuhakikisha usalama na kuimarisha imani ya mtandao.

SOMA: Serikali yaunga mkono ushirikiano Airtel, ZCTV

“Tunaendelea kukuza ujumuishaji wa kifedha na kuunganisha jamii nyingi zaidi barani Afrika,” amesema.

Airtel Africa imeshukuru wafanyakazi na wadau wote kwa mchango wao katika kuhakikisha ukuaji endelevu na huduma bora kwa wateja nchini Tanzania na kwingineko.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button