Ajali ya New Force 12 wajeruhiwa Bwawani

BASI la New Force lililokuwa likitokea Tunduma kuelekea Dar es Salaam limepata ajali katika eneo la Bwawani, Chalinze mkoani Pwani baada ya kuacha njia na kugonga mti leo Februari 20, 2025 saa 11 asubuhi.
Inasemekana kuwa basi hilo likiwa barabarani ghafla liliacha njia na kuhama uelekeo na kwenda kugonga mti pembezoni mwa baarabara. Majeruhi wamefikishwa katika Hospitali ya Msoga iliyopo Chalinze kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.
Akithibitisha kuwepo kwa ajali hiyo Kaimu Kamanda, ACP Muhudhwari Msuya amesema majeruhi waliopatikana ni 12 ambao waliofokishwa katika Hospitali ya Msoga kwa matibabu na baada ya kupatiwa matibabu na majeruhi 11 tayari wameruhusiwa na alieyebaki hospitali ni mmoja ambaye anaendelea kupatiwa matibabu na hakuna kifo kilicho ripotiwa.
Kwa upande wa abiri wengine walio kuwepo katika ajali hiyo walikfaulishwa na kuendelea na safari



