Ajali yaua 20 Limpopo

TAKRIBANI watu 20 wamefariki nchini Afrika Kusini baada ya kutokea ajali barabarani katika jimbo la kaskazini la Limpopo.

Waathirika wa ajali wanaoaminika kuwa ni wachimba madini walikuwa kwenye basi ambalo lilianguka na kugongana uso kwa uso na lori.

Watu hao walikuwa wakisafirishwa kwenda kwenye migodi mikubwa ya almasi inayomilikiwa na kampuni kubwa ya madini ya De Beers.

Advertisement

Venetia, karibu na mipaka na Botswana na Zimbabwe, inachangia zaidi ya 40% ya uzalishaji wa almasi wa kila mwaka wa Afrika Kusini.

4 comments

Comments are closed.